YANGA inaendelea na mazoezi yake hapa kisiwani Pemba, tayari kwa kuwavaa watani wao Simba kesho Jumamosi, lakini katika mazoezi yao ya juzi jioni na jana Alhamisi makocha Hans Pluijm na Boniface Mkwasa walifanya zoezi moja kubwa la kukaba tu na kushambulia.
Katika mazoezi yao yanayofanyika katika Uwanja wa Gombani, Pluijm na Mkwasa waligawanya vikosi vitatu vilivyokuwa vikipishana kila baada ya dakika 15 ambapo kila mchezaji alitakiwa kumkaba mwenzake zoezi lililoashiria ukabaji unaohitajika Jumamosi.
Mkwasa ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu katika zoezi hilo, ambapo alikuwa mkali kila alipokuwa akimuona mchezaji yeyote akifanya uvivu wa kukaba huku mara unapopata mpira jukumu la kushambulia linaanza mara moja.
MATTEO AKIONA
Zoezi hilo liliendana na adhabu mbalimbali kwa waliofanya uzembe na straika Matteo Simon alikumbana na adhabu ya kupiga ‘pushapu’ 15 baada ya kuzembea kukaba Oscar Joshua aliyekwenda kufunga kirahisi bila ya kukabwa na mshambuliaji huyo.
Uchuguzi wa Mwanaspoti umebaini kwamba kufanyika kwa zoezi hilo makocha hao waligundua udhaifu wa kikosi chao katika kukaba kwa nguvu mara wanapopoteza mpira kitu abacho kingeweza kuwapa madhara katika mchezo dhidi ya Simba.
COUTINHO AMSHTUA PLUIJM
Ishara ya kuingia kwa dozi hiyo ni kitendo cha kukaba kwa nguvu kwa kiungo Andrey Coutinho ambaye alikabidhiwa kukabana na Yondani, ambapo wakati Yondani akienda kufunga Coutinho licha ya kuonekana yuko hoi alikimbia na kumpokonya mpira beki huyo kitu ambacho kilimvutia Pluijm na kumpongeza wa kumtamkia; “Vizuri Coutinho leo umefanya kitu ambacho sijawahi kukiona tangu nimekujua, safii”.
WAJAZWA PUMZI
Achana na zoezi hilo la juzi kabla ya mazoezi hayo katika mazoezi ya siku ya Jumanne kikosi Pluijm na Mkwasa nusura wapasue mapafu ya wachezaji hao baada ya kuwakimbiza kwa muda mrefu.
Chanzo:Mwanaspoti
Chanzo:Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment