5. Jamie Carragher (Liverpool – michezo 737, magoli 5)
Beki huyo wa zamani England alicheza michezo 737 akiwa na Liverpool. Carragher (37) alishinda makombe mawili ya FA, kombe la vijana la FA, makombe mawili ya ligi na mawili ya ngao ya jamii. Pia alishinda kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mara mbili, UEFA Cup na makombe mawili ya Super Cup.
Gary Neville (Manchester United – Michezo 602, magoli 7)
Kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Uingereza kwa sasa, ni mwanachama wa United darasa la 92. Aliitumikia Man U kwa misimu 19 na kuchukua kila kombe ambalo mchezaji alihitaji kuwa nalo katika ngazi ya klabu. Beki huyo wa zamani ameshinda makombe 20, ikijumuisha makombe nane ya EPL, FA matatu, makombe mawili ya ligi, Matatu ya ngao ya jamii, moja la Intercontinental, kombe la dunia kwa vilabu na makombe mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Alikipiga kwa Mashetani Wekundu kuanzia mwaka 1992-2011.
Tony Adams (Arsenal – Michezo 672, magoli 48)
Mchezaji huyo wa zamani wa Uingereza alitumia miaka yake yote ya soka kukipiga katika klabu ya Arsenal kama beki wa kati. Tangu mwaka 1983 mpaka 2002 akiwa na Arsenal, Adams alishinda makombe manne ya ligi kuu, makombe matatu ya FA, makombe mawili ya ligi, kombe la washindi la UEFA , na makombe matatu ya Ngao ya Jamii.
Katika maisha yake yote ya soka akiwa katika dimba la Highbury, Adams alikuwa nahodha wa Arsenal kwa takribani miaka 14.
Paul Scholes (Manchester United – michezon 718, magoli 155 )
Akichukuliwa kama moja ya wachezaji wenye vipaji vikubwa sana kuwahi kutokea katika taifa la Uingereza. Katika misimu ishirini aliyochezea klabu ya Manchester United, Mpishi huyo wa mabao wa zamani wa England alichukua makombe yakiwemo makombe saba ya EPL, Matatu ya FA, mawili ya Ligi, matano ya ngao ya jamii, moja la Intercontinental Cup, moja la klabu bingwa ya dunia na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na tuzo nyingine binafsi.
Ryan Giggs (Manchester United –michezo 963, magoli 168 )
Giggs ni mchezaji mwenye historia ya kipekee zaidi Uingereza baada ya kutumia miaka yake yote 24 ya soka kukipiga katika ligi kuu Uingereza kwenye klabu ya Man United.
Kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Wales ameshinda makombe 34 yakiwemo kumi na tatu ya Ligi Kuu Uingereza, manne ya FA, matatu ya Ligi, tisa ya Ngao ya Jamii, moja la UEFA Super Cup, moja la Intercontinental Cup, moja la Klabu Bingwa ya Dunia na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pia nashikilia rekodi ya klabu ya kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi na wa sita katika orodha ya wafungaji wa muda wote wa klabu.
0 comments:
Post a Comment