MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, huenda akaukosa mchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu baada ya kuumia enka juzi katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tambwe aliyeifungia bao la pili timu yake hiyo katika dakika 45, alitoka dakika ya 84 baada ya kuumia nanafasi yake kuchukuliwa na Malimi Busungu.
Mshambuliaji huyo amelimbia BINGWA jijini jana kwamba ameumia enka na mguu umevimba hivyo huenda akakosa mchezo huo kwani bado hajapewa taarifa kamili na daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani.
Alisema kwa sasa ni mapema kuzungumzia suala la muda gani atakuwa nje ya uwanja, lakini anachofikiria huenda kesho asijiunge na wanzake.
“Juzi niliumia enka hivyo mguu umevimba kidogo, sidhani kama kesho (leo) nitafanya mazoezi na wenzangu, pia sijajua kama nitacheza mchezo wa Jumamosi, nasubiri taarifa kutoka kwa daktari,” alisema.
0 comments:
Post a Comment