Yanga na Simba wote wapo mawindoni kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mara nyingi timu hizi zinapokaribia kukutana huwa kunakuwa na vitimbi vya hapa na pale, sasa basi, katika pita yangu nimekutana na hii posti kwenye ukurasa maarufu wa mashabiki wa Yanga unaojulikana kwa jina la 'Naipenda Yanga', wameandika hivi;
"Waandishi na makachero wa Simba wanahaha kupata taarifa kuhusu Yanga lakini uongozi umekubaliana kutoongea chochote,kambi ipo chini ya ulinzi mkali hakuna mtu anayeruhusiwa kupiga picha wala kuhojiana na wachezaji. .
Wakipigiwa Simu wanajibu hivi :-
Jerry Murro "Nipo kwenye kikao nitafute muda mwingine" toka jumanne yupo kikao ama msibani.
Mzee Akilimali "Mimi sio msemaji wa Yanga,hata kama ni katibu wa baraza la wazee kwani hao wazee wanacheza namba ngapi?mimi nipo busy na kampeni nitafute baada ya octoba 25 kumbuka mpanda punda wawili huchanika msamba,kwa heri"
Katibu Mkuu Dr .Jonas Tiboroha namba yake iliyozoeleka haipatikani. . Na ukijaribu kuifuata timu Pemba huko ndo moto utakutana na meneja wetu Hafidh Saleh hana mzaha hata kidogo utabaki kuichungulia timu kwa mbali. . Tumeamua kutoongea ongea ila ushindi wa kesho ndio utaongea.
Kubwa zaidi leo timu inarejea Dar kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Simba"
0 comments:
Post a Comment