Emmanuel Adebayor aliishutumu familia yake kumroga ili acheze chini ya kiwango.
Wachezaji wengi wa ngazi za juu wa Kiafrika wanaochezea ligi kuu Uingereza inasemekana wanaamini sana katika nguvu za giza kupata mafanikio katika soka.
Ripoti kutoka gazeti la the Sun zinadai kwamba wachezaji hao nyota wanaoamini katika hilo hutumia maelfu ya pauni kuwapa waganga wa kienyeji ili kuwapandisha viwango vyao
Wachezaji hao huenda kwa wapiga juju huko Afrika Magharibi, ambapo huoneshwa namna ya kufanya mambo ya miujiza ambayo pia husemekana kuondoa mikosi hasa ya majeraha ya mara kwa mara kwa wachezaji hao.
Mwanzoni kabisa mwa mwaka huu mchezaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor alimshuku mama yake kutumia nguvu za uchawi kumroga ili asiweze kupacika mabao pindi awapo uwanjani.
Hata hivyo, mshambuliaji wa zamani wa West Brom Brown Ideye amewaonya baadhi ya mastaa hao kwa kuamini katika nguvu hizo
Ideye alisema: “Nafahamu baadhi ya wachezaji ambao hutumia nguvu hizo lakini hawafanikiwi. Huu ni upuuzi tu. Wanaweza kupata mafanikio ya muda mfupi, lakini huwagharimu katika kipindi kirefu cha maisha yao. Waganga wana ushawishi mkubwa sana.
“Mara zote hawa ni watu ambao hujitahidi kujitafutia utajiri kwa njia zisizo halali kwa kukuambia uongo.
“Kama mambo kama haya yangekuwa yanafanyika, basi leo hii badala ya Messi na Ronaldo kuwa wanashinda kila siku uchezaji bora wa dunia, ingekuwa ni kwa wachezaji wa Kiafrika.
Baadhi ya uchawi hugharimu mpa Yuro 460 kwa mara moja.
0 comments:
Post a Comment