10. Harry Kane- Tottenham Hotspur
Alifunga mabao 36 katika michezo 81 aliyoichezea Spurs . Ana umri wa miaka 22 kwa sasa.
9. Edinson Cavani- Paris Saint-Germain
Amefunga magoli 56 katika michezo 96 aliyoichezea PSG kwa michuano yote licha ya kutocheza michezo mingine mingi tu.
8. Alexis Sanchez- Arsenal FC
Amefunga magoli 25 katika michezo 53 kwa michuano yote ambayo ameichezea Arsenal huku akitupia mabao 47 ndani ya michezo 141 akiwa na FC Barcelona. Huyu ni moja ya wachezaji wanaojituma sana katika ulimwengu wa soka hivi sasa.
7. Diego Costa- Chelsea FC
Alifunga mabao 22 ndani ya michezo 40 msimu uliopita akiwa na Chelsea. Akiwa Atletico Madrid alifunga mabao 64 ndani ya michezo 135.
6. Wayne Rooney- Manchester United.
Amefunga mabao 233 katika michezo 485 aliyocheza akiwa na klabu yake Manchester United. Japo kiwango chake kwa sasa si cha kuridhisha lakini bado ni miongoni mwa washambuaji hatari ulimwenguni kwa sasa
5. Zlatan Ibrahimovic-PSG.
Amefunga magoli 106 ndani ya michezo 126 akiwa na PSG katika michuano yote.
4. Karim Benzema-Real Madrid
Amefunga magoli 134 kwenye michezo 282 akiwa na Real Madrid katika michuano yote.
3. Robert Lewandowski-Bayern Munich
Amefunga magoli 28 ndani ya michezo 54 aliyoichezea Bayern Munich. Alifunga magoli 103 ndani ya michezo 186 akiwa na Borussia Dortmund kabla ya kujiunga na Munich.
2. Luis Suarez- FC Barcelona.
Amefunga mabao 27 ndani ya michezo 48 akiwa na klabu yake mpya ya Barcelona. Pia alifunga mabao 82 ndani ya michezo 133 akiwa na Liverpool.
1. Sergio Aguero- Manchester City
Muargentina huyu sio miongoni mwa washambuliaji namba 9 warefu kama unavyodhani, lakini lakini anaifanya kazi yake vilivyo, alifanya hivyo akiwa nchini Uhisapani lakini vivyo hivyo nchini Uingereza. Amefunga magoli 108 ndani ya michezo 166 akiwa na Manchester City. Alifunga mabao 101 ndani ya michezo 234 akiwa na Atletico Madrid ya Uhisapania.
0 comments:
Post a Comment