Taifa Stars imelazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Nigeria jioni ya jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kwenye mchezo wa Kundi G wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017.
Kwenye mchezo huo Stars ilionyesha kiwango kilichopitiliza ila tu ikashindwa kuzitumia nafasi ilizotengeneza.
Kwa upande wa Nigeria hawakuweza kutengeneza nafasi yoyote ya wazi kwenye dakika zote za mchezo. Mtetezi wao alikuwa golikipa Carl Ikeme, aliyeokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Stars na kuufanya mchezo ubaki bila mabao.
Kikosi cha Taifa Stars kilionyesha kujiamini tangu dakika za mwanzoni za mchezo. Ni Thomas Ulimwengu aliyesumbua mno ngome ya Nigeria kupitia upande wa kulia kwenye dakika za mwanzo.
Mapema kwenye dakika ya 3 Ulimwengu alijaribu kumpita Kingsley Madu lakini mlinzi huyo wa Nigeria akamchezea madhambi na Stars wakatunukiwa Mpira wa adhabu ambao haukuweza kuzaa matunda yoyote.
Timu ziliendelea kushabuliana kwa zamu lakini Stars walionekana kuutawala mchezo zaidi. Kwenye dakika ya 21 Mrisho Ngassa alitishia kumpita Kenneth Omeruo lakini mlinzi huyo alimchezea madhambi na mwamuzi akaamuru mpira wa adhabu upigwe.
Mbwana Samatta alipiga mpira ule wa adhabu kwenye dakika ya 22. Shuti lake kali lililokuwa likielekea wavuni lilipanguliwa na golikipa Ikeme.
0 comments:
Post a Comment