MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma, amesema amejitoa kwenye vita ya kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora msimu huu na kuwaachia tuzo hiyo wachezaji wenzake, Amissi Tambwe na Simon Msuva.
Pamoja na kauli yake hiyo, tayari Ngoma ameshaanza kucheka na nyavu alipoifungia timu yake hiyo bao moja katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi, huku jingine likifungwa na Simon Msuva.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Ngoma alisema akili yake ipo zaidi kuisaidia Yanga kupata matokeo mazuri bila kujali kama anafunga au la.
Alisema kila kukicha anawaza kuisaidia Yanga kwa kucheza vizuri kuunda kombinesheni ya aina yake na washambuliaji wenzake, Msuva, Tambwe na wengineo, itakayokuwa moto wa kuotea mbali kwa timu pinzani.
0 comments:
Post a Comment