Rias wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akiwa na
Afisa Mtendaji Mkuuwa Azam Media, Rhys Torrington wakati wa makabidhiano ya mkataba wa kuanza michuano ya Ligi
Ya FA
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kushirikiana na Azam Media, wameanzanisha michuano ya Mpira miguuu itakayojulikana kwa “Azam Sports Federation Cup”
Shindano la hilo litatumia mfumo maarufu ambao unatumiwa nchini Uingereza katika michuano ya FA na vilevile nchini Uhispania katika michuano ya Copa del Rey nchini Hispania.
Akizindua Shindano hilo jpya kabisa wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na viongozi mbali mbali wa Kampuni ya Azam Media na wamiliki wa timu za mpira nchini kutoka madaraja yote, Malinzi amesema michuano hiyo itazishirikisha timu mbalimbali ikiwemo za Ligi Kuu ya Vodacom na timu za madaraja mengine mawili ya chini na kufanya idadi ya timu kufikia 54.
Malinzi amesema michuano hiyo itakuwa na msisimko mkubwa nchini na itakuwa huku lengo lake kubwa likiwa ni kuinua soka ambalo kimsingi limeshuka kutokana na ligi kuu kukosa timu nyingi.
Michuano hii itakuwa chachu katika kuleta msisimko wa Watanzania, hasa ukizingatia kwamba kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitaka michuano kama hii ambayo inashirikisha timu za Ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza na la pili ili kuleta hamasa katika mikoa ambayo haina timu inayoshiriki ligi kuu", alisema.
Malinzi ameongeza kuwa timu itakayochukua kombe hilo itajinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 50 pamoja na kupata nafasi ya kushiriki moja kwa moja kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Amesema endapo timu ambayo ipo ligi kuu itashika nafasi ya 1 kwenye msimamo wa Ligi, na pia ikafanikiwa kuchukua kombe la FA basi nafasi hiyo itapewa na Timu ambayo itaingia fainali kwenye michuano ya FA.
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji Mkuuwa Azam Media Rhys Torrington, amesema nia ya Kampuni yake kudhamini michuano hiyo ni kutaka kukuza mpira nchini kwa kutaka kufikia malengo.
Amesema licha ya kudhamini michuanao hiyo kwa kipindi cha Miaka 4, pia michuano hiyo itarushwa moja kwa moja kupitia Vituo vya TV vya Azam Media.
Udhamini utagharimu kiasi cha bilioni 3.3 kwa kila mwaka.
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI HIZI HAPA
17-24 RED TEAMS
1. PANONE FC – KILIMANJARO
2. POLISI DAR-ES-SALAAM –DAR-ES-SALAAM
3. POLISI – DODOMA
4. POLISI MARA –MARA
5. POLISI MOROGORO –MOROGORO
6. POLISI TABORA –TABORA
7. RHINO RANGERS – TABORA
8. RUVU SHOOTING – PWANI
9. MVUVUMA FC – KIGOMA
10. PAMBASC – MWANZA
11. SABASABS UNITED FC – MOROGORO
12. SINGIDA UNITED – SINGIDA
13. TRANSIT CAMP – DAR-ES-SALAAM
14. TOWN SMALL BOYS – RUVUMA
15. VILLA SQUAD – DAR-ES-SALAAM
16. WENDA SC – MBEYA
1-16 BLUE TEAMS
1. ABAJALO FC – DAR-ES-SALAAM
2. ABAJALO FC – TABORA
3. AFC – ARUSHA
4. ALLIANCE SCHOOLS FC – MWANZA
5. CHANGANYIKENI – DAR-ES-SALAAM
6. COCACOLA KWANZA FC –MBEYA
7. COSMOPOLITNI FC – DAR-ES-SALAAM
8. GREEN WORRIORS FC –DAR-ES-SLAAM
9. JKT RWAMKOMA FC
10. KARIAKOO SC – LINDI
11. MADINIS SC –ARUSHA
12. MAGEREZA –IRINGA
13. MKAMBA RANGERS FC – MOROGORO
14. MILAMBO SC – TABORA
15. MSHIKAMANO SC – DAR-ES-SALAAM
16. BULYANHULU FC – SHINYANGA
CREDIT:fullhabari
0 comments:
Post a Comment