Lionel Messi amepelekwa hospitali baada ya kupata mjaeraha dakika tisa tu baadaa ya mchezo wa La Liga kati ya Barcelona na Las Palmas na kupelekwa moja kwa moja hospitali.
Messi alionekana kuumia mguu wake wa kushoto katika dakika tano tu za kwanza na kujitahidi kuendelea kubaki uwanjani lakini hali ilizidi kuwa mbaya na kusababishwa kuwahishwa hospitali.
Messi akitolewa uwanjani
Kwa hali hiyo, Messi atakosa michezo miwili ya awali ya taifa lake dhidi ya Ecuador ambayo ni ya kufuzu fainali za kombe la dunia.
Vile vile kuna uwezekano mkubwa kwa mchezaji huyo kukosa mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla na mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen huku akitarajiwa kurudi katika mchezo dhidi ya Rayo Vallecano hapo Oktoba 17.
0 comments:
Post a Comment