‘Katibu mkuu wa umoja wa Matawi ya mashabiki wa Mbeya City Fc, Thimoth Mwalongo, amesema wanatarajia kuanza safari siku ya jumamosi tayari kwa kuisapoti timu yao itakayokuwa kwenye uwanja uwanja wa Chamanzi Copmlex siku ya jumapili kucheza na Azam Fc katika mchezo wa raundi ya 4 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Mapema leo Katibu huyo amedokeza kuwa kikao maalumu cha kujadili safari hiyo kitafanyika jioni leo kwenye hotel ya Apple Line iliyopo Soweto jijini Mbeya kikao ambacho kinatarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki kutoka matawi yote 14 yalipo ndani ya jiji.
“Kikao ni leo, tunajadili kuhusu safari, kama unavyojua tupo kila mahali pamoja na timu yetu hatujawahi kuicha, tunakwenda Chamanzi kwa lengo moja tu la kuisapoti timu, misimu miwili iliyopita tuliweka rekodi ya kuujaza uwanja huo, nina hakika haijawahi kuvunjwa na tunataka kuivunja wenyewe msimu huu” alisema.
Akiendelea zaidi Bwana Mwalongo ambaye pia anajulikana kwa jina la Mkandalasi aliweka wazi kuwa zaidi ya magari matano hadi saba aina ya Coaster yanatarajiwa kutumika katika kuwabeba mashabiki hao.
0 comments:
Post a Comment