Adnan Januzaj amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester United.
Dortmund imeipiku Valencia ambayo ilikuwa inamuwinda nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji.
Valencia ilijaribu kumsajili Januzaj Jumapili iliyopita, lakini walishindwa na sasa kijana ametua Dortmund.
Januzaj ali-post picha kwenye mtandao wa Twitter akiwa na jezi ya Dortmund na kuandika ujumbe usemao:
"Nimefurahia kusaini Dortmund! Naangalia msimu mpya".
Januzaj ana miaka 20, ameichezea United mechi 62 na kufunga magoli 5.
Ametwaa makombe matano ya Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment