Azam FC inaendelea na mazoezi kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara ambapo kocha mkuu wa timu, Stewart Hall amepiga 'stop' kikosi chake kucheza mechi za kirafiki na sasa ni ufundi tu hadi msimu utakapoanza.
Stewart amesema, mechi 18 ambazo ni za kirafiki pamoja na za mashindano zimetosha kabisa kujua kipimo cha wachezaji wake.
"Kwa sasa ni ufundi tu, narekebisha mambo mengine madogo madogo, hatutacheza tena mechi za kirafiki, nahitaji kuwa na kikosi changu kwanza kwa maandalizi zaidi,"Stewart aliiambia tvuti ya klabu ya Azam.
Katika mechi za kirafiki ambazo Azam FC wamecheza, wamepoteza mechi moja tu waliyofungwa na JKT Ruvu mabao 2-1 na nyingine walishinda pamoja na kutoa sare.
MECHI
Baadhi ya mechi walizocheza Azam waliifunga Friends Rangers 4-2, ilishinda mfululizo dhidi ya JKT Ruvu 1-0 Chamazi, 1-0 African Sports Tanga, 1-0 na Coastal Union Tanga.
Katika mechi za Kombe la Kagame, Azam FC ilimaliza mechi zao zote bila kufungwa hadi ilipotangazwa bingwa. Iliwafunga KCCA 1-0, Malakia ya Sudan Kusini 2-0, 5-0 Adama City ya Ethiopia, Yanga SC penalti 5-3 baada ya kutoka suluhu tasa, KCCA 1-0 na mechi ya fainali dhidi ya Gor Mahia ya Kenya walishinda 2-0
Baada ya hapo ilijichimbia Zanzibar na kucheza mechi za kirafiki ikaifunga KMKM 1-0 , Mafunzo 3-0 na JKU 2-0 kabla kupoteza kwa Yanga mchezo wao Ngao ya Hisani kwa penalti 8-7 baada ya suluhu.
Ilitoa sare ya 1-1 na Mwadui, na kufungwa na JKT Ruvu 2-1 .
0 comments:
Post a Comment