Kocha Mkuu wa mabingwa wa
kandanda Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans, Mholanzi, Hans van der
Pluijm amesema ana imani kubwa na kikosi chake na anaona kina nafasi ya kufanya
vyema katika michuano yote mwakani.
“Michuano ya nyumbani na ya
kimataifa, Yanga ina nafasi. Huenda wako wanaona kama kikosi chetu kina
upungufu. “ Amesema Pluijm na kuongeza:“Huenda ni baada ya kutolewa katika
michuano ya Kagame. Lakini wanasahau kwamba tuna kikosi bora na ambacho
hakijabadilishwa sana.
“Tunaendelea kuwaamini wachezaji wetu, tunaendelea kuyafanyia marekebisho
makosa ambayo tumefanya au yalijitokeza ili kuwa boara zaidi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment