Chelsea wameonywa kwamba wanaweza kulipa dau linalokaribia kufikia rekodi ya dunia kama wanataka kumsajili kiungo wa Juventus, Paul Pogba, wakati wa dirisha dogo la mwezi Januari mwakani.
Majira ya kiangazi mwaka huu, nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ilikuwa katika rada za Jose Mourinho ambaye aliweka mezani ofa ya paundi milioni 54, lakini .
Juventus waligoma kabisa kumuachia kijana huyo mwenye miaka 22.
Hatimaye, mkurugenzi mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta ameonya kuwa Pogba ambaye ameimarika kuwa moja ya viungo mahiri duniani ana thamani ya Euro milioni 100 sawa na paundi milioni 73.
Dau la paundi milioni 86 walilolipa Real Madrid katika usajili wa Gareth Bale kutokea Tottenham ya England, ndilo linashikilia rekodi ya dunia na Marotta anaamini dili la Pogba litakaribia mzigo huo.
"Kwa vile tunataka kushinda, tumeamua kuwabakiza wachezaji muhimu kama Pogba, ingawa tulikuwa na ofa nyingi kutoka klabu muhimu". Marotta amewaambia waandishi wa habari jana.
"Hapo baadaye atakuwa na thamani ya Euro milioni 100 (Pogba)".
Mfaransa huyo ambaye amejaaliwa kasi, nguvu na ufundi alijunga na Juventus mwaka 2012 kutokea Manchester United na ameisaidia timu yake kurudisha makali katika soka la Italia.
Juventus, mabingwa wa Serie A katika miaka minne iliyopita, wameanza msimu huu kwa kupoteza mechi mbili za kwanza na Marotta amekiri kwamba ni vigumu kupata warithi wa Andrea Pirlo, Arturo Vidal na Carlos Tevez, ambao wameondoka majira ya kiangazi.
Kwasasa Pogba yuko Ufaransa ambapo anatimiza majukumu ya timu ya Taifa ya nchi hiyo inayojiandaa na fainali za EURO 2016 zitakazofanyika nchini humo.
0 comments:
Post a Comment