Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Mshambulizi wa Taifa Stars, John Bocco amesema wachezaji wote wapo tayari kwa gemu ya Jumamosi hii dhidi ya Nigeria katika kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2017. Stars itaikaribisha ‘Super Eagles’ katika uwanja wa Taifa.
“Kwa upande wetu sisi kama wachezaji tuko tayari kwa mechi. Tumefanya maandalizi mazuri, mwalimu amekuwa akitupatia mbinu tofauti za kuweza kuwakabili Nigeria. Wachezaji tumekuwa tukimsikiliza na kuyafanyia kazi maelekezo yake. Kwanza nitangulize shukrani zetu kama wachezaji kwa mashabiki wetu”, amesema Bocco.
“Kabla ya kucheza na Uganda (kufuzu CHAN) tulikuwa tukipigwa na mawe, tunazomewa kila tunapopita. Watanzania walikata kabisa tamaa na timu yao ya Taifa lakini sasa tunaona wamerudisha moyo wao na tunachoweza kuwaambia wasivunjike moyo, watuamini kama wanavyotuamini kwa sasa, tutapigana Jumamosi ili kushinda gemu yetu”.
0 comments:
Post a Comment