Wednesday, September 30, 2015

Kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall amesema wakati kikosi chake kitakapokuwa kinapambana na Coastal Union leo kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, nahodha wa kikosi hicho John Bocco ataanzia benchi kwasababu anasumbuliwa na goti baada ya kuumia kwenye mchezo ulipopita dhidi ya Mbeya City.
Mtandao huu umefanya mahojiano na Stewart Hall ili kutaka kujua hali ya Bocco kisaikolojia na kama yuko tayari kuendelea kucheza kwenye kikosi cha Azam kwenye michezo ya hivi karibuni inayokikabili kikosi hicho.
“Nahodha wetu John Bocco ataanzia benchi kwenye mchezo wa kesho, lakini kuanzia kwake benchi hakuhusiani na tukio lililotokea kwenye mechi iliyopita bali anasumbuliwa na matatizo ya goti ambayo alipata kwenye mechi iliyopita wakati tunacheza na Mbeya City”, amesema Hall.
“Tukio lililotokea kwenye mchezo uliopita la mchezaji wa Mbeya City kumdhalilisha mchezaji wetu ni la aibu kubwa na halifai kufanywa na mchezaji wa ngazi ya ligi kuu. Matokeo yake badala ya watu kujadili mchezo wa Azam dhidi ya Mbeya City mchezo uliokuwa mkali na wenye upinzani mkubwa, wamehama na kuanza kujadili tukio hilo ambalo ni la aibu”.
“Lakini tunashukuru kitendo hicho kimeonekana na TFF wameshatoa kauli yao japo haikuwa rasmi kuhusu mchezaji aliyehusika na udhalilishaji wa aibu kwa aina ya mchezaji mwenyewe ambae amejiaibisha pia yeye pamoja na timu yake”.
“Club yetu inawataalamu wengi wa kila aina pamoja na wanasaikolojia ambao tayari wamekaa na mchezaji na kuzungumza nae, tunashukuru Bocco yuko vizuri na ametuhakikishia kuwa yuko tayari kuendelea kucheza”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video