Lionel Messi anaweza kukaa nje ya uwanja mpaka wiki nane baada ya kupata jeraha la goti kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Las Palmas uliopigwa leo hii.
Messi aliliazimika kutolewa nje mnamo dakika ya nane tu baada ya kuonekana kupata jeraha hilo baada ya kugongana na beki wa Las Palmas Pedro Bigas mnamo dakika ya tatu ya mchezo.
Lionel Messi akiugulia maumivu baada ya kugongana ana beki wa Las Palmas Pedro Bigas leo hii.
Kipa wa Las Palmas Javi Varas akijaribu kumuangalia Messi baada ya kugongana na beki wa timu hiyo Pedro Bigas.
Messi alichukuliwa na kupelekwa moja kwa moja katika hospitali ya Clínica Cruz Blanca na majibu kueleza kuwa kuna mpishano wa mifupa.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique alisema: 'Majeraha ni kitu kibaya sana katika mpira wa miguu duniani lakini ni mbaya zaidi hasa ikiwa ni kwa Messi.
0 comments:
Post a Comment