Sunday, September 27, 2015

Mfungaji wa goli la kwanza la Azam FC Mudathir Yahya (kushoto) akishangilia goli lake na mchezaji mwenzake Farid Mussa 
Mfungaji wa goli la kwanza la Azam FC Mudathir Yahya (kushoto) akishangilia goli lake na mchezaji mwenzake Farid Mussa

Kikosi cha Azam kimeendelea kushinda mechi zake mfululizo kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya leo kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam walianza kufunga goli lao dakika ya tisa kipindi cha kwanza kupitia kwa Mudathir Yahya aliyepokea pasi kutoka kwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kisha kupiga shuti ambalo lilimgonga beki wa Mbeya City na mpira kuambaa kwenye eneo la hatari la Mbeya City ambapo Mudathir akaachia tena shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Hadi kpindi cha kwanza kinamalizika Azam FC walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya Wagonga nyundo wa jiji la Mbeya.

Kipindi cha pili City waliingia na makali mapya huku wakishambulia kwa pamoja na kulifanya lango la Azam kuwa kwenye presha kubwa, wakati Mbeya City wakilisakama lango la wapinzani wao, ndipo Azam walicheza ‘counter attack’  ya haraka wakati wachezaji wote wa Mbeya City wakiwa golini kwa Azam. Sure boy alipiga pasi ndefu iliyomkuta Kipre Tchetche ambaye alimpiga chenga golikipa wa City na kuukwamisha mpira wavuni kuiandikia Azam goli la pili.

Mbeya City waliendelea kufanya mashambulizi ambayo mwisho wa siku yalizaa matunda kwani Raphael Alpha aliipatia timu yake ya Mbeya City goli la kufutia machozi

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video