Wednesday, August 5, 2015

Beki wa Yanga Joseph Zutah (kulia) akiwania mpira na Ibrahim Amin wa Khartoum National Club kwenye mchzo wa kombe la Kagame hivi karibuni
Klabu ya Yanga huenda ikaachana na beki wake wa kulia mghana Joseph Zutah kutokana na kushindwa kuonesha kiwango ambacho kilikuwa kinatarajiwa na timu hiyo kwa mechi ambazo amecheza akiwa kwenye klabu hiyo hadi sasa na inadaiwa Yanga wanafanya mpango wa kumtafutia timu ya kujiunganayo mapema kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara.
Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema wapo kwenye mazungumzo na mchezaji huyo na kama watafikia makubaliano basi ataenda kujiunga na klabu nyingine ambayo hakuitaja.
“Kuna ‘business’ ambayo inaendelea huenda Zutah akaenda kuchezea timu nyingine (mkataba juu ya mkataba) lakini sio kwamba tumemtupia virago. Kuna timu mbili za nje ya nchi ambazo zimeonesha ‘interest’ ambapo klabu hizo zilituma maombi ya kumpata mchezaji huyo kwenye klabu aliyotoka halafu hiyo klabu ya zamani ya Zutah ikatutumia sisi (Yanga)”.
“Na ilikua ni nafasi ambayo mchezaji mwenyewe alikuwa anaitaka sana, sasa tumeona ni afadhali tukae nae tuongee tuone kama anaweza kwenda kule na sisi tuone inakuaje”.
Zutah amesajiliwa na Yanga miezi michache iliyopita akitokea nchini Ghana lakini ameshindwa kuonesha ubora wake wakati wa michuano ya Kagame iliyomalizika juma lililopita ambapo Yanga ilitolewa kwenye hatua ya robo fainali na timu ya Azam kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video