Wababe wa soka mjini Madrid, Real Madrid wamethibitisha mshambuliaji wao kutoka nchini Ufaransa, Karim Benzema anasusumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja.
Uthibitisho wa taarifa za mshambuliaji huyo umelazimika kutolewa, kufuatia Benzema kutokuwepo kwenye kikosi cha Real Madrid ambacho kipo nchini Ujerumani kikishiriki michuano ya kombe la Audi.
Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya klabu hiyo nguli nchini Hispania, zimeeleza kwamba siku moja kabla ya kiklosi cha The Galacticos hakiajaanza safari kuelekea mjini Munich, Benzema alifanyiwa vipimo na alibainika kuwa na matatizo ya misuli ya paja.
Hata hivyo hatua ya mshambuliaji huyo kutokuwepo kwenye msafara wa kuelekea nchini Ujerumani, iliendelea kuchagiza tetesi za usajili wake kwenye klabu ya Arsenal ambayo inatajwa kumuwania kwa dau la zaidi ya paund million 40.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Benzema kukosa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Real Madrid kuelekea msimu mpya wa ligi huko nchini Hispania, baada ya kuachwa katika safari ya mashariki ya mbali ambapo Real Madrid waliweka kambi ya juma moja nchini China.
0 comments:
Post a Comment