Bossou (kulia) akimdhibiti Didier Drogba kwenye moja ya mechi waliyochuana
Mabingwa wa
kandanda Tanzania bara wameridhika na kiwango cha beki wao mpya, Vincent Bossou
kutoka Togo na wanatarajia kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Mkuu wa Idara na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema wanaamini kuongezeka kwa mlinzi huyo
wa kimataifa mwenye uzoefu kutaifanya timu iwe imara zaidi katika safu ya
ulinzi.
“Yanga imeridhishwa
na kiwango cha mchezaji Vicent Bassou ambaye alikuja kwetu kutoka Togo ambako
anaichezea timu ya Taifa” Amesema Muro na kuongeza: “Jana alicheza mchezo wake,
japokuwa alipumzishwa, lakini sisi kama klabu tumeamua kuingia naye mkataka wa
miaka miwili na ataanza kuitumikia rasmi klabu katika michuano ijayo ya ligi kuu Vodacom Tanzana bara na michuano
ya kimataifa”.
“Sisi kama
Yanga tunaamini tunavyozidi kwenda mbele, ndivyo mchezaji huyu atazidi kupata
fursa ya kukaa na wenzie na kuzoeana na kujenga timu ya mfumo wa pamoja”.
0 comments:
Post a Comment