Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Kila mwanadamu huzaliwa akiwa na ‘ kipawa’ Fulani, nje ya elimu ya darasani kipaji husika kinaweza kuendesha maisha ya mtu kuanzia umri wa ujana wake hadi uzeeni. Pengine Mungu hajatupa haraka mafanikio tunayohitaji lakini naamini bado amekuwa mwema kwetu sisi wanadamu kwa kutupa ‘ njia ya milele ya kuishi’. Unaweza kujiuliza ‘ Ni Kipi chenye Kasoro- Viumbe u dunia na usipate jibu la moja kwa moja kumaanisha kile ulichohitaji kufahamu.
Nimeshiriki katika mpira wa miguu kwa nusu ya maisha, kama kijana mwingne yeyote mwenye mtazamo wa kufanikiwa kupitia kipaji cha ska name ni mingni mwa. Lakini wakati mwingine mataraji yanafikia kikomo na kukubali ukweli kuwa wakati umepita na hata ukisimamisha majira, muda utaendelea kusonga mbele.
Kwa Mtanzania yeyote mpenzi wa kandanda atakuwa na ufahamu kuhusu Simba SC na Yanga ( Licha ya ukongwe wa klabu hizi mbili ndiyo kubwa zaidi na zenye mafanikio nchini. Ni klabu hasimu zaidi za soka nchini Tanzania-pia ni ‘ Watani wa Jadi’. Nakumbuka wakati nasoma katika Shule za msingi, Somanda, Bariadi, Kibondo na Kabwigwa kisha Sekondari ya Kigoma kote huko nimewahi kushiriki michezo isiyo rasmi ya ‘ Simba na Yanga’ na mashabiki walichukia kama timu ya itapoteza.
Msingi wa ‘ Mipamban ya Dar es Salaam derby’ ilijengwa katika misingi imara nyakati za uklni wa Mwingereza katika iliykuwa Tanganyika. Yanga ndiy klabu ya kwanza kuanzishwa nchini, ilisajiliwa rasmi mwaka 1935 kisha mwaka mmja baadaye Simba SC ikazaliwa ikitka ubavuni mwa Yanga baada ya baadhi ya Wazungu kujitenga na kwenda kuanzisha klabu ya Sunderland.
Yanga imejijenga katika msingi wa ‘ timu ya wananchi’ ambao walikuwa upande wa kupigania uhuru na Simba imekuwa ni klabu ya watu Fulani ‘ matajiri’ ambao wali rithi timu kutoka katika ‘ mabaki ya Waingereza’. Nguvu ya Yanga na Simba ni kubwa kwa sababu klabu hizo zimejijenga katika misingi imara mbele ya Watanzania.
Kuna wakati nilipata kuzungumza kwa kirefu ya Mzee Hamis Kilomoni, naye akanikumbusha tuki mja ambalo lilitokea baada ya mwamuzi , Ndimbo Manyota ( sasa Marehemu) kuisaidia Yanga kuishinda Simba kwa mabao 2-1 jijini Mwanza. Sikumbuki vizuri kama ni lile pambano la kihistoria ambalo pia tumiekuta katika uwanja wa Nyamagana ama sivyo, ila nachtaka ufahamu kuwa aliyekuwa Rais wa nchini wakati huo, Baba wa Taifa, Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusimamisha msafara wake ili tu kuwapisha mashabiki wa Simba ambao walikwenda kwa wingi kuipokea timu ya pale Stesheni ya Treni, Posta.
Mzee Kilomoni aliniambia kuwa, Mwalimu aliposimamisha msafara wake akamuuliza aliyekuwa Waziri Mkuu, Mzee Rashid Mfaume Kawawa kuwa ‘ Haya Maandam ni ya nini?’, Mzee Kawawa akamjibu kuwa ‘ Ni Mashabiki wa Simba wamekuja kuipkea timu ya kutka Mwanza’.
Mwalimu, Mungu amrehemu alikuwa mdadisi na mtu mwenye mtazam mpana sana, akamuuliza tena Mzee Kawawa, ‘ Kwani Simba wameshinda kombe gani?’. Akajibiwa kuwa ‘ Wamefungwa juzi na Yanga’, mwalimu akashangaa! Wamefungwa, alafu mashabiki wameujaza mji!. Akaelezewa mazingira ya mechi ilivyokuwa.
Katika mchezo huo Simba ilingoza hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika lakini Mwamuzi, Manyota kwa kuwa alikuwa ‘ Mnazi wa kutupwa’ wa Yanga akaendelea kuchezesha mechi na Yanga wakasawaisha kisha dakika ya 110 wakafunga goli la ushindi. Mwalimu akamwambia Mzee Kawawa, afanye vyovyote kuhakikisha chaguzi zote za klabu za michezo nchini zinasimamiwa na Serikali. Huku akimalizia kwa kusema, ‘ Tusipokuwa makini ipo siku kingozi wa Yanga au Simba atakuwa Rais wa Nchi.hii’
Nguvu ya klabu hizi ipo kuanzia Shuleni hadi katika Ikulu ya Rais wa Tanzania hivyo si rahisi kuzimaliza. Kenya walijaribu kuzipiga vita Gor Mahia na FC Leopards na timu hizo zilivyoporomoka katika madaraja ya chini mpira wan chi hiyo haukuwa na mvuto tena hadi zilipkuja kurejeshwa na Mheshimiwa Raila odinga baada ya kuingia madarakani kama Waziri Mkuu wa Serikali ya Kenya.
Kumekuwa na manen mengi kuwa timu hizi mbili ndiyo sababu ya mpira wa Tanzania kudumaa, lakini wanasahau kuwa bado hakujawahi kutkea kingozi makini katika ngazi yoyote ile ya mpira lakini kama klabu hizo zitapata watu makini hakika mpira utapiga hatua lakini si kwa kuziombea ‘ kifo’. Kwa sasa mpira wa Tanzania unaonekana kukilimbiliwa na wadhamini mbalimbali, watu binafsi, taasisi na makampuni hivyo kumekuwa na ngezeko kubwa la kipato.
Mathalani Itazame, Azam FC, sifikirii kama inaweza kuwa ‘ dhaifu’ kama Mtibwa Sugar hivi sasa . Mtibwa ilipanda ligi ya juu mwaka 1997 na wakashinda ubingwa wa kwanza wa nchi miaka miwili baadae kisha wakautetea mwaka 2000. Mtibwa ilikuwa klabu bora Tanzania kwa miaka mitano mfululizo kwani walishinda mataji mawili ya ligi kuu huku wakimaliza ndani ya ‘ 3 Bora’ kuanzia 1999-2004.
Ilikuwa klabu makini katika usajili, Mtibwa ilikuwa ikisaini wachezaji bora wa Simba na Yanga na klabu nyingine za ligi kuu na walita upinzani mkali kwa vigogo Simba na Yanga. Azam FC ambayo ilianzishwa mwaka 2007 na kupanda ligi kuu mwaka uliofuata ilijipangia malengo ya kuwatengeneza wacheza’;ji wake vijana na tuliona mafaniki ya miaka ya 2009-2011, lakini wakaingia katika mtazamo wa kusaini wachezaji hata walishuka viwango ilimradi tu walikuwa nyota miaka ya nyuma.
Stahili yao y a usajili iliwasaidia kukua haraka kwa na kuishinda Mtibwa katika Tatu Bora. Imejijenga hivyo daima na kufikia mwaka huu wametengeneza uhasama mkubwa sana na klabu bingwa mara nyingi zaidi nchini, Yanga SC. Katika mipambano 15 iliyopita timu hizo zimefungana mara Tano Tano ( ukiachana na ushindi wa mikwaju ya penalty ambao Azam waliupata katika Robo Fainali ya Kagame Cup mapema mwezi uliopita)
Yanga imeishinda Azam FC mara mbili katika michezo ya Ngao ya Jamii ( Yanga 1-0 Azam, 2013, Yanga 3-0 Azam, 2014) na mara moja wameishinda katika mchezo wa fainali wa Kagame Cup, 2012. Katika miaka mitatu mfululizo timu hizo zimekutana katika mchezo wa Kikombe na mara zote Yanga wameshinda, mwishoni mwa wiki hii watakutana kwa mara ya Nne na Azam wamejinasibu kuwa watashinda kwa mara ya kwanza ili kuongeza mataji katika makabati yao.
Azam imeshinda vikombe vya Mapinduzi, Ligi kuu na klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ndani ya miaka mitatu hii ambayo klabu kubwa kama Simba ikiwa inasotea kuingia mingoni mwa timu mbili za juu. Simba imepoteza makali kiasi cha kupungua mvuto kwa wapenzi wa kandanda na wapenzi wa timu hiyo wamekuwa wakifurika kwa wingi wakati Yanga ikicheza na Azam na licha ya kutoonesha wazi kuwa ‘ wanaisapoti Azam FC pindi ikicheza na Yanga’ lakini kiukweli kabisa wamekuwa na mwamko wa kuishangilia Azam kwa sababu imekuwa ikiwanyanyasa mahasimu wao kila wanapokutana.
Yanga SC vs Azam FC si Zaidi ya Simba na Yanga kwa sababu mashabiki hawajiti fahamu kama zinapkutana klabu hiz kubwa nchini. Baada ya miaka miwili au mitatu pamban la Yanga na Azam litakaribia lile la ‘ Dar es Salaam derby’ kwa kuwa tayari wananchi wamekuwa wakitka mikani na kuja kutazama pamban hil lakini lile la Simba na Yanga ni kubwa zaidi kwa maana linahusisha hadi mashabiki wan je ya nchi huku lilikwa na burudani na matuki mengi ya kukumbukwa.
Katika hadhi ya kimpira, Yanga SC vs Azam FC ndiyo pambano bora zaidi kwa sasa Tanzania. Pambano awali lilikuwa linahusisha mashabiki wengi wa Yanga na wachache wa Azam FC lakini baada ya Yanga kupigwa 3-1 na kurusha Ngumi Machi, 2012 mechi baina ya timu hizo imekuwa ya Visasi na upinzani mkali Nje na Ndani ya uwanja. Simba na Yanga zina mizizi na misingi imara lakini Azam wanazidi kutengeneza ndoto ya baadhi ya wapenzi wa mpira nchini ambao wanatamani kuona klabu hizo mbili zikiwa timu za kawaida. Mechi baina ya timu hizo inazidi kutanuka na kubeba hisia za watu wengi wa kandanda nchini.
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment