Arsene Wenger amesisitiza kuwa kwa upande wa takwimu, Francis Coquelin moja ya viungo bora wa ulinzi barani Ulaya.
Coquelin ametokea kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal katika miezi ya hivi karibuni, kufuatia ujio wake kutoka klabu ya Charlton Athletic mwezi Desemba ambapo alikuwa akikipiga kwa mkopo.
Mfaransa huyo ameshacheza michezo mitatu mikubwa ya ligi kuu Uingereza mpaka sasa msimu huu, lakini alikosolewa na machambuzi wa kituo cha Televisheni cha Sky Sports Gary Neville katika maandalizi ya mchez0 dhidi ya Liverpool, ambapo walitoka suluhu, lakini Wenger amemkingia kifua na kusema kinda wake huyo ni mchezaji maridadi.
Kwa uhakika kabisa, Wenger anaamini kwa namna takwimu zinayoonesha, basi Coquelin ni mchezaji bora ulimwenguni katika nafasi yake.
“Coquelin ana takwimu nzuri sana kwenye upande wa eneo kiungo wa ulinzi barani Ulaya. Nadhani huwa mnaangalia mpira kama ambavyo huwa naangalia. Mimi sijui watu huwa wanaona nini. Kwa upande wa ulinzi, Coquelin anafanya kazi kubwa sana”, Wenger aliwaambia waaandishi.
“Hebu angalia, siku zote sipo kinyume na maoni ya mtu. Watu wanaweza kusema kwamba hawadhani kwamba Arsenal ni timu bora. Nakubaliana nao. Lakini ni hatari sana kusema kwamba 'Kamwe yule hawezi kuwa mchezaji’ — hasa maoni hayo yanapotoka kwa watu wanaoufahamu mpira.
“Ndio, mimi hainiudhi hata kidogo, lakini ninachokisema hapa ni kwamba, hii inaongeza msukumo kwa wachezaji. Naamini kwamba tupo katika shughuli za kimpira na tutapambana tu.
"Watu ambao wamekuwa katika mchezo huu, napenda namna wanavyoenda kwenye televisheni kuuchambua mpira zaidi. Lakini ningependa wawasaidie watu kuupenda mpira na sio kuuchukia mpira”.
Takwimu zake Coquelin hizi hapa;
0 comments:
Post a Comment