Arsenal ndio klabu ambayo imeanza na mfumo wa mazoezi ya kufunga magoli baada ya wachezaji kuwa na kizunguzungu .
Mfumo huo unahusisha kuuzunguka mpira mara 13 kabla ya kwenda kupiga penati na kuhakikisha mchezaji anafunga goli. Zoezi hilo ni maalum kwa ajili ya kampeni ya 'Save the Children'
Wanandiga maarufu wa zamani ambao kwa sasa ni wachambuzi kama vile Michael Owen na Gary Lineker pia walifanya zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa, lakini zoezi hilo kwa upande wa Arsenal limekuwa ni la kuvutia na kuburudisha zaidi.
Theo Walcott alishindwa kabisa kuufikia mpira baada tu ya kuanguka kabla ya kuinuka na kuupiga tena mpira ambao hata hivyo ulikuwa na kasi ndogo zaidi.
0 comments:
Post a Comment