Sunday, August 2, 2015


Na Frank Mgunga
Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.
Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.

Kabla ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa vijijini.

Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA Dokta Vera Piroth akitoa hotuba yake ya kipee ambayo ilikuwa katika mtindo wa hadithi pamoja na maswali.
Pia filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na zinafanya kazi kama kioo kwa jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.

Filamu ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake.

 Producer wa filamu ya Aisha Bwana Emil Shivji akizungumza na wananchi waliohudhuria viwanja vya Bomani.
Watu wangefumbia macho mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.

Filamu hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu.

AISHA imeongozwa na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa ushirikiano na Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na Swiss Development Cooperation (SDC) na usimamiwa na shirika la UZIKWASA.

 shamra shamra za ngongoti zikikaribisha wageni waalikwa kwenye uwanja wa Bomani wilayani pangani palipofanyika uzinduzi wa flamu ya Aisha.

Msanii mahiri katika uimbaji, Vitalis Maembe alikuwepo kwenye uzinduzi wa filamu ya Aisha, alitoa burudani ya kipekee





 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video