Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mlinda-lango, Juma Kaseja Juma, 30, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Mbeya City FC ya jijini, Mbeya. Juma amekuwa ' adimu' katika viwanja vya soka Tanzania tangu alipojiunga na Yanga SC, Desemba, 2013.
Mchezaji huyo wa zamani wa Moro United na Simba SC amekuwa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja aada ya kugomea kuwekwa benchi katika timu ya Yanga. Wakati anasaini Yanga kwa mara ya kama mchezaji, Juma alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita baada ya kumalizika kwa mkataba wake na klabu ya Simba SC mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2012/13 na aliweka kipengele cha kuwa kipa chaguo la kwanza katika timu hiyo.
Alifanya makosa katika kipigo cha Yanga 1-3 Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, 2013. Alirudishiwa mpira na mlinzi, Mbuyu Twite na wakati anaumiliki tayari mchezaji wa Simba, Awadh Juma alikuwa amemfikia na hivyo akajaribu kumpiga chenga jambo ambalo lilishindikana na Awadh anaupora mpira na kufunga goli la tatu kwa timu yake.
KIPAJI KISICHOTETEREKA
Juma alijiunga na Moro United akiwa U17 mwaka 2000 akitokea Shule ya sekondari ya Makongo. Alichezea Moro kwa miaka miwili hadi aliposajiliwa na Simba SC mwishoni mwa mwaka 2002. Alikuwa kipa chaguo la kwanza kwa kipindi cha miaka nane mfululizo akiwa na klabu za Moro United na Simba.
Kati ya mwaka 2000-08, Kaseja hakutoka midomoni mwetu. Hadi anasajiliwa na Yanga kwa usajili wa rekodi Tanzania, Agosti, 2008 ( dola 30,000) mchezaji huyo alikuwa tayari ameshinda mataji matatu ya ligi kuu Tanzania Bara akiwa na Simba ( 2003, 2004 na 2007).
Kwa miaka sita mfululizo alikuwa kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Juma alijumuhishwa kama mchezaji wa timu ya Taifa kwa mara ya kwanza mwaka 2001 katika timu iliyoshinda ubingwa wa Castle Cup. Aliendelea kuwa mchezaji muhimu hadi mwaka 2007.
KWANI YANGA SC WALIMSAINI KASEJA, 2008 KWA USAJILI GHALI?.
Alitajwa kama ' hirizi ya bahati ya Simba' katika mipambano ya mahasimu hao-Dar es Salaam derby. Kumbuka kuwa, Yanga imewahi kusubiri kwa miaka nane mfululizo ili kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Simba katika michezo ya ligi kuu Bara.
Kati ya mwaka 2000-08, Simba haikuwahi kupoteza pambano dhidi ya Yanga na walikuja kuruhusu hilo mara tu baada ya Kaseja kuhamia Yanga katikati ya mwaka 2008 huku ukiwa usajili wa kwanza wa gharama kubwa katika mpira wa Tanzania. Licha ya kuvuta zaidi ya milioni 35, Juma alisaini mkataba kama mchezaji hasa wa kulipwa.
Mshahara usiopungua milioni moja kwa Mwezi, nyumba na gari la kutembelea. Usajili ule uliwafungua macho wachezaji wengi ambao kwa wakati huo walikuwa wakisainiwa kwa pesa zisizozidi milioni 10-15. Yanga walitumia kiasi kikubwa mno cha pesa ili kumtoa Kaseja katika lango la Simba kwani ndiye alibaki tatizo kwao baada ya Suleimani Matola na Primus Kasonso kuondoka katika timu hiyo.
Haukuwa usajili wa kimpira na haukuwa mapendekezo ya kocha Mserbia, Dusan Kondic kwa kuwa tayari alikuwa na Ivo Mapunda na alipendekeza kusajiliwa kwa Mserbia mwenzake, Obren ambaye ndiye alidaka katika ushindi wa Yanga 1-0 Simba, Oktoba, 2008 ambao ulikuwa ni wa kwanza kwa Yanga mbele ya Simba tangu mwaka 2000.
Juma alikuwa benchi la Yanga siku hiyo licha ya kuanza msimu kama golikipa chaguo la kwanza mbele ya Obren. Taratibu, Dusan akaanza kumuweka benchi Kaseja na Obren akapewa kipaumbele hadi na mashabiki wa klabu yake hadi, April, 2009 baada ya Yanga kupoteza 3-0 ugenini dhidi ya Al Ahly ya Misri. Juma akaidakia Yanga katika
Atakumbukwa Yanga kwa mazuri machache kama ' ufutaji wa mikwaju miwili ya penalti' katika mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Azam FC ambao ulimalizika kwa ushindi wa 3-2 walioupata Azam. Katika mchezo huo matokeo ya sare yangeishusha daraja Azam FC na hadi mapumziko walikuwa nyuma kwa mabao 2-0.
Kaseja alifunga goli la umbali mrefu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Aliamua kuachana na ofa ya mkataba mpya katika timu hiyo na kurejea Simba kwa usajili ulio ghalimu milioni 30, Agosti, 2009. Ndani ya miezi 12 akawa ametengeneza zaidi ya milioni 80 huku pia akishinda mataji mawili mfululizo ya ligi kuu ( 2008/09 akiwa Yanga na 2009/10 akiwa nahodha wa Simba).
Kati ya 2009/10-2012/13 alishinda mataji mawili ya ligi kuu akiwa Simba na kufikisha jumla ya mataji 6, matano akishinda akiwa kipa chaguo la kwanza la Simba. Ameshinda zaidi ya mara tatu tuzo ya golikipa bora wa msimu, pia amewahi kushinda tuzo kadhaa za mwanasoka bora wa mwaka wa Tanzania. Juma hajawahi kutetereka, ila miaka miwili iliyopita imekuwa migumu sana kwake kwa sababu ya kukutana na changamoto nyingi za ndani na nje ya uwanja.
Amefanya kazi kubwa mfululizo na kushinda mataji akiwa timu ya Taifa na katika ngazi ya klabu. Pengine Yanga hawakuwahi kuwa na nia nzuri kwake kwani ni miongoni mwa majina ya wafungaji katika ushindi mkubwa wa mahasimu hao katika karne mpya, Simba 5-0 Yanga, Mei, 2012. Kwa maslai Juma amecheza kama Pele ametengeneza pesa nyingi akiwa Yanga timu ambayo hajaidakia hata mechi 20.
Hakuwa na bahati na Yanga kwani katika gemu mbili alizoidakia timu hiyo dhidi ya Simba ameruhusu mabao matano!. Atapiga pesa nyingine za Yanga endapo atawashinda katika kesi iliyo mahakamani hivi sasa. Yanga wamemshtaki, Juma kwa kuvunja mkataba wakati upande wa Juma unasema Yanga walikiuka makubaliano ya kimkataba kwa maana hiyo walivunja mkataba.
KWANINI CITY IMEMSAINI KASEJA?.
Baada ya Yanga kufungwa 3-1 na Simba katika Mtani Jembe, 2013 nilisema wazi; ' wakome sasa kuwasaini wachezaji wa Simba'. Wamemtajirisha, Kaseja wakati hawakuwahi kuwa na mahitaji yao. Walitaka kuifunga Simba tu ili kufuta uteja wa muda mrefu. Kwa, Mbeya City itakuwa ni tofauti. Bila shaka kikosi chao kilihitaji nyongeza ya wachezaji wazoefu na baada ya kumsaini Kaseja, Jumatano hii,
City tayari ina wachezaji washindi kama Juma Nyosso na Haruna Shamte ambao walishinda mataji ya ligi sambamba na Kaseja katika nyakati tofauti pale Simba. Ni yeye mwenyewe Kaseja anayepaswa kuwajibika ili kuingia katika kikosi cha kwanza cha Juma Mwambusi ambaye amemsaini kwa mategemeo ya kukinyanyua kikosi chake.
Kaseja ni mchezaji wa mazoezi, na wapenzi wengi wa kandana nchini wamefurahishwa na kitendo cha kipa huyo kurejea katika ligi kuu. City ni mahala sahihi kwake kwani ni timu yenye mashabiki wenye kutia hamasa mara zote. Ni klabu shindani kwa sasa katika soka la Tanzania.
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment