Monday, August 31, 2015

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Kama mshabiki wa Manchester United nimechukizwa sana na kipigo cha 2-1 kutoka kwa Swansea. Mambo mengi yamenikera, namna Batefimbi Gomes alivyofunga goli lake la 9 katika mchezo wa tisa mfululizo wa ligi kuu England. Nilichukizwa na namna nahodha, Wayne Rooney alivyopoteza mpira kirahisi na kuzaa goli la kusawazisha la Swansea lililofungwa na Andrew Ayew.
Golikipa, Sergio Romero amecheza gemu tano mfululizo lakini katika gemu yake ya sita alifungwa ' kizembe' na Gomes. Romero amekuwa mzuri katika mipira ya juu. Rooney amefunga katika gemu moja tu kati ya sita za United msimu huu. Amepoteza hali, kiwango chake pia kinaporomoka tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson. ' Ile si Manchester United'. Haina wachezaji wa England katika kikosi cha kwanza!.
Luke Shaw amekuwa na kiwango kizuri msimu huu, ana kasi na uwezo wa kutengeneza mashambulizi. Alishiriki katika goli la kuongoza lililofungwa na Juan Mata mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Criss Smalling ameendelea kuwa imara katika beki ya kati licha ya kusumbuliwa sana na washambuliaji, Ayew na Batefimbi. Rooney alikuwa Muingereza watatu kuanza katika mchezo wa jana wakati, Ashley Young na Michael Carrick wakiwa katika benchi. Sikuona sababu yoyote ya Luis Van Gaal kuwaanzisha nje kwa wakati mmoja, Carrick, Young, Marouane Fellaini na Antonio Valencia.
Mchezo wa kwanza wa Van Gaal ulikuwa ni dhidi ya Swansea ambao walipoteza 2-1 katika uwanja wa Old Trafford, Agosti, 2014. Van Gaal alikwenda Libert Stadium katika mchezo wake wa 50 na kupigwa kwa 2-1 kwa mara ya tatu mfululizo na Swansea.
United ilitengeneza mashambulizi 11, wakafunga mara moja huku mipira mitatu ikichezwa na mlinda lango wa Swansea. Kikosi cha Van Gaal kilianza na Romero, Matteo Darmatti, Bastian Schwensteiger, Morgan ambao hawakuwepo katika vichapo vya mwaka jana lakini mambo yamekuwa vilevile na United iliyomiliki mchezo kwa asilimia 64 imechapwa kwa mara ya kwanza msimu huu.
Ndiyo, kwanza ligi ya England iko katika mzunguko wa nne na United imekuwa na tabia ya kuanza msimu vibaya na kutwaa taji hilo. Ila kwa namna Van Gaal anavyochukulia ligi ya England itakuwa ngumu sana kwake na United kupata matokeo yanayotarajiwa licha ya kuwa na mkusanyiko wa wachezaji washindi na wenye ubora. Van Gaal ataanguka zaidi kama ataendelea kuwapuuza wachezaji wa Kiingereza.
Mimi si shabiki wa timu ya Taifa ya England lakini tangu 1999 nimekuwa nikitazama msingi wa mafanikio ya Manchester United na kujithibitisha kuwa wachezaji wa Kiingereza ndiyo walikuwa msingi wa mafanikio ya Ferguson na klabu kiujumla. Kama ningekuwa katika nafasi ya Van Gaal ningewaanzisha, Valencia na Young katika wing, Fellaini na Carrick katika eneo la kiungo wa kati ili kuikabili Swansea inayocheza mchezo wa kasi, nguvu. Juan Mata alifunga lakini zaidi ya hapo alizidiwa na ' miili mikubwa' ya walinzi wa Swansea.
United ilipata kona moja na mchezaji wake akaotea mara moja!. Ukiona hivyo ni wazi kuwa nguvu ya timu ilikuwa ndogo katika kupandisha mashambulizi licha ya kumiliki mpira. Swansea ilitengeneza mashambulizi 9, wakafunga mara mbili na mara mbili mlinda lango, Romero akazuia. Licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 34 tu timu hiyo ya Wales ilikuwa tishio kwa safu ya ulinzi ya United.
Wenyeji hawakupata kona yoyote lakini waliotea mara 3 kwa dakika zote 90. Kwanini Manchester United inashindwa kutengeneza mashambulizi mengi?. Van Gaal anajaribu kulazimisha timu hiyo kupanga mashambulizi yake katikati ya uwanja. Kwa ligi ya England ni Arsene Wenger pekee aliyefanikiwa, Arsenal hata ikiwa katika presha ya kushinda mechi hawabadili uchezaji wao wa kutokea katikati ya uwanja.
Carrick ni mtu maalum kwa gemu za Kiingereza pale United, Fellaini nafikiri huu ungekuwa msimu wake bora zaidi katika ligi ya England baada ya kuisaidia sana Man United kurejea top4 msimu uliopita, wawili hawa wanatakiwa kuwa kikosi cha kuanza mchezo, inaweza kuwa na Bastian au Morgan lakini kuwaweka benchi kwa pamoja ni makosa kama anavyoendelea kung'ang'ania kumchezesha Rooney katika nafasi ya mshambulizi wa kwanza.
Va Gaal ana timu nzuri sana lakini amapaswa kufanya machaguo mazuri ya wachezaji hasa kwa mechi dhidi ya wapinzani wanaocheza kwa nguvu na kasi. Kumchezesha Rooney katika nafasi ya sasa namba-9 ni sawa na kuzidi kumuweka katika wakati mgumu mchezaji huyo ndani ya uwanja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video