Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ameilazimisha PSG kulipa pauni milioni 3 za ziada kwa ajili ya kumsajili Angel Di Maria, 27, baada ya mchezaji huyo kuonekana akiwa na mmiliki wa PSG nchini Qatar (Daily Mirror), Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa Pedro, 28 kutoka Barcelona kwa pauni milioni 20 (Sun), Van Gaal katika kumshawishi Pedro amesema atampa nafasi katika safu ya ushambuliaji kushirikiana na Wayne Rooney na Memphis Depay (Daily Telegraph), Sunderland wanazungumza na Manchester United kuhusu kumsajili kwa mkopo Adnan Januzaj, 20 (Sunderland Echo), meneja wa Manchester United Louis van Gaal yuko tayari kumuanzisha kipa Sergio Romero weekend hii na kutomchezesha David De Gea (daily Star), Wolfsburg wapo tayari kumuuza kiungo wao Kevin De Bryne, 24 kwenda Manchester City lakini kwa pauni milioni 50 (Daily Mirror), wakala wa beki wa Augsburg, Baba Rahman, 21 anasema beki huyo wa kushoto anakaribia kusajiliwa na Chelsea baada ya kukubaliana maslahi binafsi (Daily Star), Chelsea pamoja na Juventus wamezungumza na Calgiari kuhusiana na kumsajili kiungo kutoka Ghana Godfred Donsah, 19 (Daily Express), West Brom wamejitokeza kumsajili kiungo wa Anderlecht Dennis Praet, 21 anayesakwa pia na Arsenal (Talksport), West Brom wameambiwa lazima watoe pauni milioni 10 kumpata winga wa QPR Matt Phillips, 23 (The Sun), West Ham wapo tayari kurejea Manchester United na kitita cha pauni milioni 12 kumtaka mshambuliaji Javier Hernandez (London Evening Standard), Chicharito pia ataomba bei yake ya pauni milioni 12 kupunguzwa, huku Tottenham pia wakimtaka (Daily Star), Liverpool huenda wakakamilisha usajili wa Alexandre Lacazette, 24, baada ya klabu yake ya Lyon kumwambia mshambuliaji huyo kuwa anaweza kuondoka (L'Equippe), Everton wana wasiwasi wa kumpoteza beki wao John Stones, 21, baada ya Chelsea kutayarisha dau la tatu la pauni milioni 30 (Daily Telegraph), Kevin Prince Boateng amewasili mjini Lisbon tayari kusaini mkataba wa miaka miwili na Sporting Lisbon (A Bola). Share tetesi hizi na wapenda soka wote.
Wednesday, August 5, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment