Wednesday, August 5, 2015

Aliyekuwa golikipa wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na vilabu vya Simba na Yanga Juma Kaseja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Jerryson Tegete huenda wakajiunga na klabu ya Mwadui FC kama mambo ya klabu hiyo yataenda kama yalivyopangwa.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema pamoja na kukamilisha usajili wa wachezaji waliokuwa wanawahitaji, lakini bado nafasi ipo kwa ajili ya Juma Kaseja na Jerry Tegete kwani wakipewa nafasi wanaweza wakaonesha uwezo mkubwa.
“Mimi nimeshamaliza usajili, nimeshasajili wachezaji 26 wanatosha, wachezaji pekee ambao kama mipango yangu itaenda sawasawa basi kuna mpango wa kuwaongeza Juma Kaseja na Jerry Tegete. Kwasababu ni wachezaji ambao nimezungumza nao na wameniambia wanataka kucheza na hawakuweka mbele kipato, mimi wamenivutia kwasababu tunapokuwa na wachezaji kwenye timu tunataka tuwatumie kucheza ili tupate mafanikio kwenye ligi”.
juma-kaseja1“Lakini kunawachezaji ambao hawaperfom inabidi tuwatoe kwenye dirisha dogo la usajili, lakini ukiwa na wachezaji wazuri wenye kuonesha commitment ambao wanataka kucheza kuisaidia timu yao sioni kwanini nisiwachukue kwasababu namba bado inatosha”.
Kwa usajili wa wachezaji wa kigeni unaofanywa na baadhi ya vilabu vya ligi kuu hapa nhini Julio amesema yeye hatishwi na usajili huo kwani yeye ni Kocha mkubwa na anatambua uwezo wa wachezaji wengi na hata pale anapowaita wachezaji haoni kama ni wazee na anatambua kuwa ni wachezaji wenye uwezo mkubwa”.
“Mimi kwanza sitishiki na usajili wa Azam, Simba na Yanga, wao wamevutika na wachezaji wao wa nje kwasababu zao binafsi kwanza wanafedha,Yanga wanatarajia wakiwa na wachezaji wa kigeni watafanikiwa kwasababu wanacheza mashindano ya Afrika wanataka kuingia kwenye ‘Super eight’ ili wafanikiwe. Mimi sidhani kama hilo litafanikiwa”.
Lakini Azam hivyohivyo nao japokuwa juzi wamechukua ubingwa wamefanya vizuri nimeona timu yao sio mbaya sana, Simba wamepoteza ubingwa kwa takribani miaka mitatu kwahiyo wanategemea wakiwa na wachezaji wa nje basi wanaweza wakafanya kile kitu wanachokitarajia na watapata ubingwa lakini sioni kama itafanikiwa vilevile”.
Msikilize Julio hapa chini akieleza nia yake ya kuwasajili Kaseja na Tegete

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video