Friday, August 28, 2015

Tambwe (kulia) na Ngoma (kushoto). 
KIPA wa zamani, mnazi mkubwa na mwanachama wa Simba mwenye utaalamu mkubwa na nafasi ya magolikipa, Idd Pazi, ameangalia safu ya ulinzi ya timu hiyo akatikisa kichwa.
Hofu yake imekuja zaidi baada ya kuangalia uzoefu wa mafowadi wa Yanga pamoja na Azam ambazo ndiyo washindani wakubwa wa Simba inayotaka kurejesha heshima yake kwenye Ligi Kuu Bara.
Pazi ambaye amewahi kucheza Simba pamoja na kuwa kocha wa makipa,  ametamka kwamba haamini kama  mlinda mlango Manyika Peter Jr, anaweza kuhimili mikikimikiki ya washambuliaji wazoefu kama Donald Ngoma, Amissi Tambwe (Yanga) pamoja na Kipre Tchetche wa Azam FC.
Pazi alielezea  anavyomfahamu Manyika Jr kwa kipindi ambacho alikuwa naye Simba, kuwa  bado alitakiwa kuwa chini ya kipa mzoefu ambaye angekuwa anamfundisha jinsi ya kuwamudu mastraika wenye mbinu kali kama Ngoma.
“Maana ya chipukizi ni yule ambaye anaendelea kujifunza mambo mengi, lakini ana kipaji, uzoefu ni jambo lingine kama alivyokuwa Ivo Mapunda Simba ama alivyo Ally Mustapha Barthez wa Yanga, hao wanaweza kutumika kwenye mechi ya aina yoyote lakini sio chipukizi kama Manyika ,” alisema.
Pia alisema ikumbukwe mechi ya Nani Mtani Jembe ambayo Simba iliibuka na ushindi dhidi ya Yanga, iliyompa chati Manyika lakini mapungufu mengi yalizibwa na aliyekuwa beki wa kikosi hicho Joseph Owino ambaye alijitahidi kuokoa hatari nyingi.
Alisema kwa staili ya uchezaji  wa Ngoma na Kipre wanatakiwa wakutane na makipa makini wenye akili nyingi na pia wasio  na mambo mengi nje ya kazi yake.
YANGA YATAMANI
ZANZIBAR
Mholanzi Hans Pluijm anataka kikosi cha Yanga kiingie mafichoni Zanzibar kwa ajili ya maandalizi zaidi ya mechi za Ligi Kuu Bara. Yanga ambayo sasa inajifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi  Kurasini, Jijini Dar es Salaam sehemu kubwa ya wachezaji wake wako kwenye timu zao za Taifa.
Pluijm alisema: Tunaendelea na maandalizi kama kawaida lakini kwa sasa tunafanya na wachezaji wa kikosi B, kama unavyojua wachezaji wangu wengi wako kwenye timu ya taifa.Lakini ninachokitaka, mara tu mechi ya Stars itakapomalizika, nataka timu iingie kambini kwa maandalizi zaidi na mahali ninapopapendekeza ni Zanzibar kwa sababu ni mahali kwenye utulivu na hakuna purukushani,”alisema Pluijm.
Kama Yanga itakwenda huko, itakutana na watani wao wa Jadi Simba ambao nao wamerudi huko. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroa amenukuliwa akisema, kikosi hicho kitakwenda kambini Zanzibar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video