Tuesday, August 18, 2015

Adi Yussuf mshambuliaji wa Tanzania anaecheza kwenye klabu ya Mansfield Town inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini England
Afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto amesema, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Adi Yussuf anaekipiga kunako klabu ya Mansfield Town inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini England, hatoungana tena na timu ya taifa kufuatia kupata majeraha wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Nottingham Forest mwishoni mwa juma lililopita.
Uongozi wa klabu yake umemuomba kocha wa timu ya Taifa Charles Boniface Mkwasa asimjumuishe mchezaji huyo kwenye kikosi cha timu ya taifa kwasababu bado anaendelea kupata matibabu chini ya usimamizi wao na kuahidi kwamba, pindi atakaporejea tena uwanjani Mkwasa atapata fursa ya kumtumia.
Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam
Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam
Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kuondoka siku ya Jumamosi  Agosti 22 usiku mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC na kuelekea nchini Oman ambako imepata mwaliko wa kucheza mechi moja ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Oman mchezo utakaochezwa jijini Muscat Agosti 24.
Baada ya timu kuondoka jijini Dar es Salaam Agosti 22 usiku, inatarajiwa kufanya mazoei siku ya tarehe 23 Agosti kujiandaa na mechi hiyo ya Agosti 24. Mara baada ya mchezo huo, timu itaondoka kuelekea Istanbul, Uturuki ambapo itaweka kambi ya siku saba ikifanya mazoezi na itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa.
Kabla ya kuelekea Oman na baadae Uturuki, kocha mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa atatangaza orodha ya wachezaji 22 watakaoondoka kuelekea huko kwa ajili ya kambi na michezo ya kirafiki kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Nigeria mechi inayotarajiwa kuchezwa Septemba 5, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa.
Kizuguto pia amezungumzia kuhusu mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumamosi Agosti 22 kwenye uwanja wa Taifa kati ya Yanga dhidi ya Azam FC, amesema maandalizi yanakwenda vizuri na yapo katika hatua za mwisho. Baada ya taratibu zote kukamilika kati ya leo na kesho, watatangaza viingilio na utaratibu mwingine unaohusu mchezo huo
Katiaka hatua nyingine, Kizuguto amevikumbusha vilabu vya soka kuwa dirisha la usajili linafugwa Alhamisi Agosti 20 mwaka huu na hakutakuwa na muda wa nyongeza hivyo vilabu vijitahidi kukamilisha usajili wao kwa muda uliosalia kwani baada ya dirisha la usajili kufungwa, vilabu vitalazimika kulipia shilingi 500,000 kwa kila mchezaji atakaesajiliwa nje ya muda.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video