Sunday, August 2, 2015

Chama cha Wacheza soka Tanzania SPUTANZA, kimewasilisha barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulitaka limtangaze mlinda mlango Juma Kaseja kuwa ni mchezaji huru.
Kaseja ambae Yanga imemfungulia mashtaka kwenye mahakama ya kazi ikitaka mchezaji huyo kuwalipa mamilioni ya shilingi wakimtuhumu kuvunja mkataba na timu hiyo.
Mwenyekiti wa SPUTANZA Mussa Kisoky amesema, tayari wameshapeleka barua TFF wakiomba imtangaze Kaseja kama mchezaji huru.
“Ni kweli Juma alikuja kwenye chama, alileta malalamiko yake kuhusu Dar Young Africans na sisi tumeshaanza kulishughulikia suala lake, tumelipeleka TFF tayari kwahiyo sisi ombi letu kwa TFF ni kuwaambia wamtangaze Juma kama mchezaji huru kutokana na taratibu zilizokuwa zimefanyika hazikufata mstari ule unaotakiwa kwenye system ya soka”, amesema Kisoky.
Awali Juma aliwaandikia Yanga barua ya kuvunja mkataba baada ya Yanga kutotekeleza baadhi ya vifungu vya mkataba hasa kipengele kinachohusu ada ya usajili ambapo Yanga walikuwa wamekiuka makubaliano na yeye akaamua kuvunja mkata.  Lakini wakati anafanya hivyo, tayari Yanga walikuwa wamemuwekea pesa kwenye akaunti yake.
Lakini ikumbuikwe kuwa, Yanga kupitia kwa mwanasheria wao Frank Chacha ilishasema Kaseja yuko huru kujiunga na klabu yoyote akisema kwamba, wanachokitaka Yanga kutoka kwa Kaseja ni madai yao ya kuvunjwa kwa mkataba, “Yanga imeshazungumza na golikipa huyo pamoja na wakili wake kwamba akitaka barua ya kuondoka Yanga ‘release letter’ wao wako tayari kumpatia lakini suala la kesi litabaki palepale”, alisema Chacha miezi kadhaa iliyopita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video