Uongozi wa Yanga SC umefurahishwa na kambi ya siku nane
waliyoweka mkoani Mbeya, huku wakicheza mechi tatu za kirafiki ambazo
wameshinda zote.
Yanga walianza kushinda 4-1 dhidi ya Kimondo FC, wakaichapa
2-0 Tanzania Prisons na jana wameichakaza 3-2 klabu ya Mbeya City FC.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
amesema mazoezi waliyofanya Mbeya yameleta tija kwao na kikosi kipo salama
,licha ya nyota watatu kusumbuliwa na marelia.
“Viongozi wa Yanga wanapenda kuwashukuru wachezaji na benchi
la ufundi kwa kazi nzuri waliyoifanya katika michezo ya kirafiki kule Mbeya.
Tumepata ushindi mzuri kabisa, siku zote nane ambazo Yanga imekuwa Mbeya,
tumekuwa na wakati mzuri, tumekuwa na mazoezi mazuri ambayo yameisaidia klabu”.Amesema
Muro na kusisitiza: “Kikosi kitatua muda wowote Dar es salaam ili kuzoea joto
la Dar es salaam, tutaweka kambi kwa
muda wote mpaka hapo tutakapoingia kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam FC”
“Hatuna ‘serious Injuries’, wachezaji wetu wako fiti,
isipokuwa ni changamoto ya hali ya hewa iliyowakuta wachezaji wetu watatu,
Nadri Haroub ‘Cannavaro’, Amissi Tambwe na Oscar Joshua, wote wana marelia
ambayo imesababishwa na muingiliano wa hali ya hewa”.
Hata hivyo, Muro amesema wachezahi hao wamepewa mapumziko, ingawa watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoingia kambini.
Yanga na Azam FC zitapambana katika mchezo wa Ngao ya Jamii
utaochezwa Agosti 22 mwaka huu uwanja wa Taifa ikiwa ni kuashiria kufunguliwa
rasmi kwa msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment