Hispania imekuwa nchi ya kwanza kuwa na timu tano zilizofuzu katika hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya Valencia kuwatungua Monaco kwa uwiano wa mabao 4-3 katika hatua ya mtoano.
Valencia almaarufu Los Che, ambao walishika nafasi ya pili katika michuano hiyo mwaka 2000 na 2001, wanaungana na timu nyingine za Uhisapania ambazo ni: Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid, huku Sevilla ambao walishika nafasi ya tano katika La Liga wameingia moja kwa moja baada ya kuibuka mabingwa wa ligi ya Europa mapema kabisa mwaka huu.
Alvaro Negredo ndio shujaa wa Valencia baada ya kuwafungia goli muhimu la ugenini na kuwapa nafasi hiyo ya kufuzu licha ya kufungwa 2-1. Negredo alianza kufunga dakika ya nne kabla ya Andrea Raggi kuwasawazishia wenyeji dakika ya 17 na Elderson Echiejile kufunga la pili dakika ya 75.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Alvaro Negredo akishangilia goli lake muhumi la ugenini lililoiwezesha Valencia kuitupa nje Monaco na kufuzu hatua ya makundi Klabu Bingwa Ulaya.
Negredo akijaribu kumtoka beki wa Monaco Ricardo Carvalho
Wachezaji wa Valencia wakishangilia
0 comments:
Post a Comment