Msafara wa Mabingwa wa kandanda nchini Tanzania, Dar es salaamYoung Africans ukiwa na viongozi,wachezaji na benchi la ufundi umeondoka leo saa 12 alfajiri kuelekea Mbeya.
Yanga itapitiliza moja kwa moja mpaka Mbozi ambako siku ya jumapili (kesho) itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kimondo FC na mapato yote ya mchezo huo yatachukuliwa na Kimondo FC.
Baada ya mchezo huo timu itaelekea Tukuyu kwa ajili ya kambi,itarudi Mbeya Mjini katika dimba la Sokoine zaidi ya mara 2 kukabiliana na Zesco ya Zambia pamoja na Big Bullets ya Malawi,bila kuusahau mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbeya City.
Haya yote ni maandalizi ya ligi kuu bara msimu 2015-2016 na dhidi ya Azam FC katika mtanange wa Ngao ya Jamii.
0 comments:
Post a Comment