Kocha mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr amemteua mshambuliaji mkongwe wa klabu hiyo, Musa Hassan Mgosi kuwa nahodha mpya.
Akizungumza na MPENJA SPORTS mchana huu, kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amethibitisha uteuzi huo na kusema kwamba waliokuwa manahodha wa klabu hiyo, Hassan Isihaka na Jonas Mkude wanatakiwa kuendelea kujifunza kwa nahodha mpya ambaye ana uzoefu mkubwa.
"Kocha ameangalia uzoefu, nahodha anatakiwa mtu kama Mgosi, anaweza kuongea na wachezaji, anahamasisha timu, ndio maana ameteuliwa".
"Timu inaweza kuwa na manahodha wanne, lakini Isihaka na Mkude wataendelea kujifunza kwa Mgosi, pindi anapoondoka wataweza kurithi nafasi yake". Amefafanua Matola.
Kwa upande wake, Mgosi amefurahia uteuzi huo na kuahidi kuunganisha timu.
"Majukumu yangu ni kuunganisha timu pamoja, kocha ameangalia uzoefu wangu, bila shaka nitaifanya kazi hiyo ipasavyo". Amesema Mgosi.
0 comments:
Post a Comment