Kocha wa Chelsea Jose Mourinho hatetemeshwi na hali ya klabu yake kutofanya usajili wa nguvu mpaka sasa ukifananisha na wapinzani wake ambao wameonekana kutumia fedha nyingi kuimarisha vikosi vyao.
Mpaka sasa Chelsea wameziba mapengo ya Drogba na Petr Cech ambao nafasi zao zimejazwa na Asmir Begovic na Radamel Falcao, ambao pia ndio wachezaji pekee waliosajiliwa na Chelsea.
Wapinzani wao wametumia mamilioni ya shilingi ikiwepo pauni milioni 49 ambayo Man City wametoa ili kunasa saini ya Sterling, lakini Mourinho bado anaamini hahitaji nyongeza katika kikosi chake.
"Ni hatari sana", aliwaambia waandishi wakati alipoulizwa kuhusu ukoefu wa majina mapya ndani ya Stamford Bridge.
"Nadhani mnachosema ni sahihi, kuna msemo unaosema: 'mchelea mwana utakuta mwana si wako'. Ni sahihi, lakini watu hao hao wnaweza kuanguka.
"Huhitaji kununua watu 10 ili kuwa na timu bora. Unaweza kuwa na timu bora kwa kuongeza mchezaji mmoja au wawili tu, ukichanganya na waliokuwepo basi mambo safi kabisa".
0 comments:
Post a Comment