Thursday, August 6, 2015

Simba SC jana usiku imechuana na KMKM ya Zanzibar katika mfululizo wa mechi za kirafiki Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar ambako wamejichimbia kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania bara.
Karibu uongozi wote wa juu wa Simba, ulifika kisiwani Unguja kushuhudia kikosi chao chini ya Muingereza Dylan Kerr kikishinda 3-2 dhidi ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo.
KMKM ndio walikuwa wa kwanza kufunga magoli yote mawili kupitia kwa mchezaji wao Mateo Antony Simon akifunga magoli hayo dakika ya 20 na 25 ya mchezo huo lakini Hamisi Kiiza ‘Diego’ akaipatia Simba goli la kwanza dakika ya 42 kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko huku KMKM ikiwa mbele kwa goli 2-1.
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi kubwa na KMKM wakaonekana wakiwa wamechoka na kushindwa kuendana na kasi ya Simba, ambapo mshambuliaji chipukizi wa Simba Ibrahih Ajib aliifungia klabu yake mabao mawili ya harakaharaka dakika ya 75 na 78 akaipa ushindi klabu hiyo wa goli 3-2. Mabao hayo yakiwa yamechangiwa na kiungo Mwinyi Kazimoto na kiungo aliyesajiliwa kutoka Zimbabwe Jastice Majiva.

Leo Simba inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam ambako ilicheza mechi tano za kirafiki ikiwa visiwani Zanzibar. 
Mchezo wa kwanza Simba ilishinda kwa goli 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar, mechi ya pili Simba ikashinda kwa goli  4-0 wakati mchezo wa tatu ilicheza dhidi ya Polisi ya Zanzibar na kushinda kwa goli 2-0 huku mchezo wake wa nne ikishinda pia kwa goli 3-0 mbele ya Jang’ombe na kumaliza na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya KMKM.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video