Monday, August 31, 2015

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Simba SC imekamilisha michezo ya maandalizi Zanzibar kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mafunzo. Washambuliaji, Daniel Lyanga, Musa Hassan Mgosi, Peter Mwalyanzi na Hamis Kizza wote walicheza katika mchezo huo wa kirafiki. Mwalyanzi na Mganda, Kizza walifunga mabao mawili kati ya matatu yaliyopatikana.
Mwalimu raia wa England, Kerry ni kama hana kikosi cha kwanza. Kwa muda wa miezi miwili ambayo amekinoa kikosi cha timu hiyo, Kerry alipaswa kuwa na orodha ya wachezaji 7-9 ambao wataunda kikosi cha kwanza.
Zikiwa zimesalia siku 12 kabla ya timu yake kucheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Africans Sport katika uwanja wa Mkwakwani, Kerry hapaswi tena kuwekeza akili/mawazo yake kuhusu usajili wa mshambulizi mpya na badala yake anapaswa kuwatengeneza vijana, Ibrahim Ajibu na Lyanga ambao kwa mtazamo wangu ni wafungaji ambao wakiaminiwa watafunga magoli katika ligi kuu msimu ujao.
Lyanga amewahi kuwa mmoja wa wafungaji bora watano misimu miwili iliyopita akiwa Coastal Union kabla ya kutimkia nchini DR Congo ambako alijiunga na FC Lupopo. Alicheza kwa dakika 45 katika mchezo wa jana na alishiriki katika goli la kwanza lililofungwa na Mwalyanzi.
Mchezaji huyo anapaswa kuongeza mazoezi ili awe 'fit' zaidi. Ajibu tayari ametuonesha uwezo wake. Vijana hawa wakinolewa vizuri wataisaidia sana Simba ambayo imekosa  mshambulizi mwingine wa kimataifa.
Mwalyanzi, Mgosi na Kizza hawa pia ni wachezaji wapya ndiyo maana nasisitiza umefika wakati wa mwalimu wa timu kuhakikisha timu inafunga kwa kuwa klabu imewasaini washambuaji wanne wapya. Kama tetesi za kurejea kwa Paul Kiongera zitakuwa habari kamili hilo ni jambo zuri zaidi kwa sababu mchezaji wa ‘  tofauti’ atakuwa ameongezeka katika timu lakini naye atakuwa mzigo kama mwalimu Kerry ataendelea kushindwa kuwapa mbinu za kufunga magoli.
Mimi ni mtu mwenye shaka kuhusu uwezo wa ufundishaji wa Muingereza huyo hasa baada ya kushindwa kupata kikosi cha kwanza hadi sasa. Kama atafanikiwa kuwajenga Lyanga na Ajibu atafanikiwa pia katika kazi yake lakini kitendo cha timu kushindwa kufunga katika ligi kitawapandisha zaidi hasira mashabiki ambao wameshuhudia utawala ukifanya uzembe katika kuhakikisha wanapata mfungaji wa uhakika baada ya kuondoka kwa Mganda, Emmanuel okwi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video