Tuesday, August 4, 2015

WATAIPENDA! Simba imeanza kunoga baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr, kupata kombinesheni kali ya Simon Sserunkuma, Ibrahim Ajibu, Hamis Kiiza na Mussa Hassan ‘Mgosi’.
Simba wameweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikianzia na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya AFC Leopard ya Kenya utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kombinesheni ya Sserunkuma, Ajibu, Kiiza na Mgosi, imemkuna mno Kerr kutokana na uelewano wao walioonyesha katika mazoezi yake yanayoendelea visiwani humo.
Katika mazoezi hayo, Sserunkuma ameonekana kubadilika kwa kiwango cha hali ya juu, baada ya ujio wa Kerr aliyeanza kuifundisha timu hiyo mwezi uliopita.
Wachezaji wengine wanaoonekana watakuwa ni tishio kwenye kikosi hicho cha Simba ni mshambuliaji mpya, Kiiza aliyesajiliwa na klabu hiyo baada ya kuachwa na Yanga kabla ya msimu uliopita.
Wengine ni Elias Maguri na Jonas Mkude ambao wameendelea kuonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi ya timu hiyo.
Akizungumza na BINGWA, Kerr alisema kulingana na jinsi alivyoridhika na hatua ya kwanza ya programu yake na ameanza kutengeneza kombinesheni kwa kila mchezaji.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video