Beki wa kati wa Azam FC, Muivory Coast Serge Wawa amesema, anajisikia mwenye bahati kuwa mmoja wa wachezaji walioipa heshima ya Ubingwa wa Kagame Cup klabu hiyo ambayo inakuwa kwa kasi.
Wawa amesema, siyo kwamba ni mara ya kwanza kwake lakini anafurahia kwa sababu ya historia hiyo aliyoitengeneza kwenye timu iliyoanzishwa mwaka 2004.
"Hii ni mara ya pili kuchukua Kombe hili kwa sababu ubingwa kama huu niliupata kwenye mashindano yaliyofanyikaa Kigali, Rwanda mimi nilikuwa naichezea El Merreihk ya Sudani,"alisema Wawa.
"Kinachonifurahisha ni historia, Azam FC ilikuwa haijawahi kuchuku ubingwa lakini nikiwa mmoja wa wachezaji hao, tumefanikiwa."
“Cha kufurahisha zaidi ni kwamba, tumechukua ubingwa bila kufungwa goli hata moja ndani ya dakika 90 mechi zote sita za Kagame Cup mimi nikiwa sehemu ya ukuta wa chuma wa klabu yetu” alitamba Wawa
AINGIA MKATABA MPYA NA AZAM FC
Wakati huo huo Serge Wawa Pascal leo ameingia kandarasi mpya na Azam FC itakayomuweka klabuni hapo hadi msumu wa 2016/17.
Wakala wa Wawa Samuel Joel aliwasili nchini jana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Azam FC kisha leo asubuhi kuingia mkataba mpya. Dili hili limevikata maini vilabu vilivyokuwa vikifanya hila za kutaka kumhamisha wawa toka Azam FC
0 comments:
Post a Comment