Droo ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imefanyika jana makao makuu ya UEFA, mjini Nyon, Uswisi.
Manchester United imepangwa na Club Brugge ya Ubelgiji na lazima iifunge timu hiyo katika mechi mbili ili itinge hatua ya makundi ya Uefa Champions League.
Kikosi hicho cha Louis van Gaal kilichomaliza nafasi ya nne msimu uliopita kitacheza mechi ya kwanza Old Trafford kati ya Agosti 18 au 19 mwaka huu.
Agosti 25 au 26 watacheza mechi ya marudiano katika uwaja wa Jan Breydel, Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment