Friday, August 28, 2015

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Makundi ya ligi ya mabingwa barani ulaya yamepangwa AlhamisI hii jijini, Monaco Ufaransa. Timu 32 Bora zimegawanywa katika makundi Nane. Timu mbili za juu katika kila kundi zitafuzu kwa hatua ya 16 Bora, timu ya Tatu katika kila kundi itaangukia katika michuano ya Europa League wakati ile itakayomaliza nafasi ya mwisho katika makundi itakuwa imemaliza safari ya michuano ya ulaya kwa msimu wa 2015/16.
Mabingwa watetezi FC Barcelona ya Hispania, mabingwa wa miaka miwili iliyopita FC Bayern Munich ya Ujerumani, Mabingwa wa mwaka jana, Real Madrid ya Hispania na mabingwa wa 2011/12 Chelsea ya England ni baadhi ya klabu kubwa zilizopangwa katika makundi ‘ rahisi’. Mabingwa hao wa miaka minne mfululizo iliyopita wanapewa nafasi kubwa ya kutingia hatua ya 16 bora licha ya kukutana na timu zenye uzoefu katika michuano hiyo……

HII NI TATHIMINI YANGU FUPI KUHUSU MAKUNDI YA MABINGWA ULAYA…..
KUNDI A; Real Madrid, Paris Saint German, Shakhtar Donetsk, Malmo FF
Real na PSG zinaweza kufuzu kama washindi wawili bora katika kundi, lakini Shakthar ambayo imempoteza mshambulizi wake Mbrazil, Luiz Adriano aliyefunga mabao Tisa msimu uliopita na kiungo ,Mbrazil, Douglas Costa si timu ya kubeza. Timu hiyo ya Ukrane imekuwa ikivuka hatua ya makundi na wakati mwingine kuingia miongoni mwa klabu nane bora  inaweza kuendeleza tabia yao ya kuvuka hatua ya makundi mbele ya vigogo hao.
Itakuwa ni  ‘ aibu’ kwa meneja yeyote kati ya Rafael Benitez wa Real au Laurent Blanc wa PSG kama klabu mojawapo itashindwa kuvuka katika kundi hili la kwanza. Klabu zote zimevuka hatua hiyo kwa misimu minne mfululizo kushindwa kufanya hivyo dhidi ya Malmo ya Sweden inayocheza kwa mara ya pili au Shakhtar itakuwa sawa na kufeli. Hakuna mwalimu atakayepona kati ya Rafa na Blanc.
KUNDI B; PSV Eindhoven, ,Manchester United, CSKA Moscow, VFL Wolfsburg
Katika urejeo wa Manchester United barani ulaya, klabu hiyo ya England ni kama ‘ imeangukia’ katika ‘ kundi la msahama’. United ambayo imeichapa jumla ya mabao 7-1 Club Brugge ya Ubelgiji katika hatua ya mtoano itamaliza kama vinara wa kundi hili mbele ya mabingwa wa Holland, PSV ambayo imerejea pia baada ya kusubiri kwa miaka zaidi ya saba.
CSKA, VFL ni timu ambazo ziliwahi kupangwa pamoja na United msimu wa 2009/10, klabu hizo za Urusi na Ujerumani zitajaribu kupambana ili kufuzu kwa hatua ya 16 Bora lakini ndani yake zitatiana pembe kuwania nafasi ya tatu itakayowapeleka Europa League.

KUNDI C; Benfica, Atletico Madrid, Garatasaray, FK Astana
Makamu bingwa wa ulaya na mabingwa wa Hispania msimu wa 2013/14 Atletico italazimika kuwashinda mabingwa wa Ureno, Benfica ili kumaliza kama washindi wa kundi la tatu. Galatasaray itabidi ipambane mbele ya timu ya Kazkhstan, FK Astana ambayo ilishanga katika hatua ya ‘ play off’. Nafasi ya tatu itakuwa ‘ target’ ya kwanza kwa Astana na wanaweza kuipata kwa kuwa Gala si klabu kali hata katika ligi ya Uturuki kwa sasa.

KUNDI D; Juventus, Manchester City, Sevilla, Borussia Monchenglabach
‘ Kundi la Kifo’. Makamu bingwa watetezi na mabingwa mara nne mfululizo wa ‘ Scudetto’ Juventus ya Italia itapaswa kuvuka kundi hili ili kuthibitisha nguvu yao mpya barani ulaya. Kwa sasa Juve imempoteza mfungaji wao bora kwa misimu mitatu iliyopita, Muargentina Carlos Tevez lakini wataendelea kupata huduma ya kijana Alvaro Morata huku wakiwa na washambuaji wapya kama Mario Mandzukic, Kingsley Coman, Simone Padon na wazoefu wengine wengi.
Ubora pekee hautatosha kwa City kuvuka kundi hili. Sevilla ni mabingwa mara mbili mfululizo wa ligi ya ulaya, na Moncheinglabach ni timu iliyofanya vizuri katika ligi ya Bundesliga msimu uliopita. Juve na Sevilla zitafuzu kama washindi wawili wa kundi wakati City italazimika kupambana na Wajerumani kuichukua nafasi ya Tatu. Ni kundi gumu kwa hakika, ni kielelezo cha michuano.

KUNDI E; FC Barcelona, Bayer 04 Leverkusen, AS Roma, Bate Borisov
Barca itakutana na upinzani mkali katika kundi hili lakini watavuka kama washindi wa kwanza. Ubora, vipaji, mbinu ni sababu ambazo zitawafanya mabingwa watetezi kufuzu kwa hatua ya 16 bora. Roma imewasaini wachezaji wakali kama Luiz Adriano na Eden Dzeko watataka kusahihisha makosa ya msimu uliopita waliposhindwa kuvuka hatua ya makundi.
Leverkusen walifika hatua ya 16 bora msimu uliopita na wametinga hatua ya makundi kwa kuichapa jumla ya mabao 3-1 SS Lazio ya Italia. BATE watajaribu kupigania nafasi ya tatu na wanawrza kuipata. Hawa ni mabingwa mara 10 mfululizo wa Beralus si wa kudharauliwa.

KUNDI F; Bayern Munich, Arsenal, Olympiacos, Dinamo Zagreb
Arsenal imetolewa mara mbili na Bayern Munich kati ya mara nne ambazo wameshindwa kuvuka hatua ya 16 Bora, wamepangwa pamoja katika hatua ya makundi na kulifanya kundi E kuwa na timu mbilizi mbili ‘ nzito’. Zote mbili, Bayern na Arsenal zimekuwa na faida ya kupangwa na timu za kawaida. Mabingwa wa Ugiriki, Olympiacos watapambana na Zagreb kuwania nafasi ya Tatu ili kufuzu kwa ligi ya ulaya.

KUNDI G; Chelsea, FC Porto, Dynamo Kiev, Maccab Tel-Aviv
Jose Mourinho atarejea kuikabili timu iliyompatia ubingwa wake wa kwanza wa ulaya, FC Porto. Chelsea imekuwa na bahati ya kupangwa kundi rahisi licha ya kuwa na mabingwa wa Ukraine, Dynamo Kiev na wale wa Israel Maccabi Tel-Aviv. Chelsea na Porto zitapambana kuwania nafasi mbili za juu wakati Kiev watalazimika kuwadhinda Maccabi ili kumaliza nafasi ya tatu.

KUNDI H; Zenit St.Petrsburg, Lyon, Valencia, KAA Gent
Mabingwa wa Ubelgiji KAA Gent wamejikuta wakipangwa katika kundi gumu sambamba na timu zoefu ulaya. Lyon ya Ufaransa imerejea katika michuano hiyo baada ya misimu sita kupita. Mabingwa wa Urussi, Zenit watachukua nafasi ya kwanza katika kundi hili, vita kubwa itakuwa kati ya makamu bingwa wa miaka ya 2000 na 2001 Valencia na mabingwa mara saba mfululizo wa zamani wa Ligue 1, Lyon.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video