Ligi kuu England msimu wa 2015/2016 inaanza leo na timu zote 20 zinakabiliwa na mechi 38.
Mabingwa watetezi, Chelsea wanafungua dimba na Swansea City.
Hata hivyo mtandao wa bwin umeleta takwimu za timu za England zinazoenesha matokeo ya mechi za ufunguzi.
Historia inaonesha kwamba Chelsea ndio klabu yenye rekodi nzuri ya kufanya vyema kwenye mechi za ufunguzi.
Katika mechi 23 za ufunguzi wa EPL walizocheza, Chelsea wameshinda michezo 15, sare tano na kupoteza tatu, huku wakifunga magoli 48.
Tazama picha chini;
0 comments:
Post a Comment