Thursday, August 6, 2015

Vincent Bossou (kulia) akipambana na Didier Drogba wakati wa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) mechi iliyokuwa kati ya Togo na Ivory Coast kwenye dimba la Royal Bofokeng Stadium Januari 22, 2013 Rustenburg, Afrika Kusini
Leo asubuhi Yanga imemsajili beki wa kati Vicncent Bossou ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Togo ikiwa bado masaa machache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili ambapo dirisha hilo litafungwa leo saa 6:00 usiku.
Beki huyo alianza soka lake kwenye klabu ya Maranatha FC mwaka 2006 na kudumu kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2009 akicheza jumla ya mechi 77 na kuifungia klabu hiyo magoli matano (5).
Vincent Bossou 2January 2010 alijiunga na klabu ya Etoile Sportive du Sahel kwa mkataba wa miaka miwili lakini mkataba wake ukavunjwa baada ya miezi mitatu baadae akiwa ameichezea klabu hiyo mechi tatu tu, na Bossou akarudi tena Maranatha FC Machi 18, 2010.
May 2011 Bossou alijiunga na klabu ya Navibank Saigon F.C ya Vietnam ambapo alicheza mechi 35 akiwa na timu hiyo na kufanikiwa kufunga magoli matatu (3) na kwa sasa alikuwa na mkataba na klabu ya Govang Hi FC ya Korea Kusini.
Vincent Bossou 3
Bossou alikuwepo kwenye kikosi cha Togo ambacho kilijitoa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2010 baada ya basi la timu hiyo kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wakati wanawasili nchini Angola ambako ndipo mahindando hayo yalifanyika kwa mwaka huo wa 2010.
Ameshaichezea timu ya taifa ya Togo kwenye michezo ipatayo 25 hajafanikiwa kufunga goli hata moja kwa mechi zote alizocheza.
Wasifu wake
Taarifa binafsi:
Jina kamili: Vincent Bossou
Tarehe ya kuzaliwa: Februari 7, 1986 (miaka 29)
Sehemu alikozaliwa: Kara, Togo
Urefu: mita 1.86 (futi 6 na inchi 1)
Nafasi anayocheza: Beki wa kati
Taarifa zinazo husu klabu
Klabu anayocheza sasa: Yanga
Orodha ya timu ambazo amewahi kucheza, idadi ya mechi alizocheza na magoli aliofunga.
MwakaTimuMechi alizochezaMagoli aliyofunga
2006-2009Maranatha FC77(5)
2010ES Sahel3(0)
2010-2011Maranatha FC23(3)
2011-2012 Navibank Saigon35(1)
2013Becamex Binh Durong 1(0)
2013TDC Binh Durong 17(0)
2014An Giang21(0)
2015Goyan Hi FC0(0)
                 Timu ya       Mechi          Magoli
                       taifa                         
2010- Togo25(0)
Yanga wamemsajili beki huyo kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu yao ya ulinzi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitumikiwa na mabeki wawili Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Kelvin Yondani ambao ubora wao unapungua kutokana na kucheza mechi nyingi kwenye timu hiyo bila kupumzika.
Vincent Bossou 1Ikumbukwe kuwa Yanga wataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa baadae mwaka huu (kombe la vilabu bingwa Afrika) hivyo wanahitaji kuwa na wachezaji wenye ubora wa kupambana kwenye michuano hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video