Azam FC wameshinda mechi ya tatu mfululizo ya kirafiki visiwani Zanzibar baada ya usiku huu kuichakaza 2-0 JKU ya visiwani humo.
Magoli ya Azam yamefungwa na John Raphael Bocco 'Adebayor' na Salum Abubakar 'sure Boy'.
Azam wanaojiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii itayochezwa Agosti 22 uwanja wa Taifa, walianza kwa kushinda 1-0 dhidi ya KMKM, wakainyuka 3-0 Mafunzo, michezo yote ikipigwa uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati wamejibu mapigo kwa Yanga ambao nao walishinda mechi tatu mfululizo za kirafiki walizocheza katika kambi yao ya siku nane mkoani Mbeya.
Yanga waliichapa 4-1 Kimondo FC, wakaifumua 2-0 Tanzania Prisons na jana wameshinda 3-2 dhidi ya Mbeya City FC.
Wote wakiwa wameshinda mechi zao tatu za kirafiki, nani ataibuka mbabe Ngao ya Jamii?
0 comments:
Post a Comment