Thursday, August 27, 2015

Kwa muda mchache anaonekana kuwa vizuri ,Francis Coquelin anaonesha kitu katika safu ya kiungo ya Arsenal. Kamati  ya uchambuzi ya espn walijaribu kuangalia kikosi cha sasa cha Arsenal na kuzungumzia kama Giroud anafaa kuanza kama mshambuliaji wa kutegemea katika mbio za kusaka ubingwa msimu huu.
Katika mechi ya Arsenal na  Liverpool iliyoisha 0-0. Arsene Wenger alikuwa mkweli kuhusu uchezaji wa timu yake msimu huu.  "Tumeanza kawaida sana.nahitaji kukiri"   baadaye stori nzima ilikuja kutokana na mechi baadhi zilizopita na kitu kilichotokea London kabla ya kipute kupigwa Emirates.
 Gary Neville alimpinga Wenger akiwa ‘ skysport’  kwa kumshutumu Wenger'kutosajili wachezaji wenye nguvu zaidi.  Akieleza kwamba inaweza ikawa ni ‘ ubishi au ujinga wa Wenger’  kwa sababu hadi sasa wanaendelea kupoteza kila siku. Walipokuwa wakijadili Wenger aliwajibu kwa staili yake akisema;
"Angalia sijui kivipi hilo linaweza kuhusiana na ujinga. Nimekuwa nikijaribu kuifanya kazi yangu vizuri kwa miaka 20 sasa. Nawaachia na watu wengne pia waweza kunijadili kuhusiana na ubora wa kazi yangu kiujumla, naweza nikakuhakikishia kuwa sio sawa ila tusiendelee na hilo suala kwa leo, usiposhinda unakosea na watu hutafuta sababu,je kuna sababu nzuri?. Nina uzoefu wa kutosha kujua unapokuwa sawa na sio sawa.” ALISEMA Wenger akimjibu Neville.
Maneno ya Neville yanaweza kuwa sawa au sio sawa, alikuwa alieleza ‘performance’  ya Arsenal kwa miaka kadhaa iliyopita, akionyesha majina ya wachezaji walioyosajilIwa tangu mwaka 2004 ilipochukua taji kwa mara ya mwisho, akionesha kwa kiasi gani wachezaji wamekuwa wa kawaida.
Lilikuwa ni suala linalojionesha lenyewe hasa pale Arsenal inapokumbana na klabu kubwa. Wenger hajawahi kumfunga Mourhinho katika ligi kuu tangu mara ya mwisho achukue ubingwa ameshnda mara 4 kwa Manchester United . Hali sasa ni tofauti kidogo, Wenger inawezekana halikuwa hajajua kuwa Nevile alikuwa sio tu anazungumzia kikosi cha sasa ambacho pia kinaonekana kuwa na wachezaj wengi wasio na nguvu
Francis coquelin ameanza mech 22 kati ya 23 za Arsenal katika ligi ya Uingereza, japokuwa tatizo lipo katika robo tatu ya mwisho ya uwanja , suala ambalo sio kawaida kwa Arsenal sababu huonekana kupunguza kasi na balance. Francis ameanza kuonekana katika msimu wa 2014/2015 baada ya kutupwa kwa mkopo Charton. Akichukua nafasi  ya Mikel Arteta kiungo tegemeo wa Arsenal anaesumbuliwa na majeraha.
Hata Wenger mwenyewe aliyekuwa na matumaini makubwa kwa wachezaj wake makinda, atakuwa ameshangazwa na uwezo wa Conguelin ambaye alisimama imara katika ushindi dhdi ya Man City 2-0 na anakuwa vizuri kila muda. Wakati Arteta akiwa na mpira wa pasi nzuri na mwenye hekima uwanjani kwa Conquelin ni tofauti.
Kijana huyo anajaribu kuwa bora zaidi katika mpira, utoaji wake wa pasi unaimairika muda hadi muda, japokuwa inasemekana pasi zake ndefu zimekuwa na mapungufu mfano baadhi ya pasi alizokuwa akimpa Ramsey zilikuwa zikizidi . Zaidi ya chochote Wenger anataka pasi bora zaidi kutoka kwa kiungo wa kati ambapo alikuwa akiweka muunganiko mzuri na Arteta wakileta nguvu na kasi kwa washambuliaji hicho ndo kinachokosekana kwa sasa.
Hili limemfanya Wenger kumrudisha Santi Carzola kama kiungo wa kati, alipokuwa akingara msimu uliopita, hii itamlazimisha Ramsey kucheza nafasi ya kulia ambayo alishawahi kuicheza . Sema Ramsey huwa hafurahii kucheza hiyo nafasi.
Ni rahisi kuelewa mawazo aliyonayo Ramsey kwani ndiyo aliyekuwa bora msimu wa 2013-2014, lakini anahamishwa nafasi kwa kosa ambalo halimuhusu. Ramsey akicheza katikati huwa  ni bora zaidi kuliko Giroud na ozil ambao mchezo wao unafanana!
Giroud ndiye anayeonekana mshambuliaji wa Arsenal kutokana na umbo lake. Mfaransa huyo sio kwamba mkaidi katika kufunga  ila anahitaji  kiungo mfungaji na ozil sio mfungaji pia, kwa hiyo Ramsey anahitajika katikati .
Imeandaliwa na Baraka Mbolembole

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video