Sergio Kun Aguero alikuwa anavaa jezi namba 16 msimu uliopita, lakini sasa amebadili ambapo atavaa jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na Edin Dzeko.
Alipoulizwa kwanini amechagua jezi hiyo?
Aguero amejibu: "Nilipofika City, Edin alikuwa anaitumia-aliitendea haki vizuri sana na kiukweli niliheshimu jambo hilo.
"Ndio maana nilichagua namba 16. Lazima nakiri, nimeifukuzia kwa miaka michache iliyopita na nina kumbukumbu muhimu na jezi namba 10, jezi hii ni maalum sana kwangu".
0 comments:
Post a Comment