Bondia Lulu Kayage akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yake ya Afrika kusini kupigana mpambano mwingine agoust 28. Picha zote na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Lulu Kayage akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yake ya Afrika kusini kupigana mpambano mwingine agoust 28.
Mdau wa mchezo wa ngumi nchini Hamissi Berege kushoto akizungumza na George Sabuni ambaye anaambatana na bondia Lulu Kayage kulia kwenda kwenye mpambano wake mwingine utakaofanyika agous 28 Afrika ya kusini.
Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa Kike Lulu Kayage amenda tena nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mpambano wake mwingine na bondia mwingine kutoka huko utakaofanyika Agost 28 nchini humo.
Akiongea kabla ya kupanda ndege, bondia huyo alijingamba kuwa anaenda huko kushinda kwa kuwa yupo fiti zaidi kwa sasa.
Alisema kuwa anaomba dua kwa Watanzania ili aweze kumchakaza Msauzi huyo tena kwa K.O mbaya kama alivyo mpiga mwenziye Lizbeth Sivhag.
Bondia huyo aliyeambatana na bondia mkongwe wa siku nyingi George Sabuni kwa ajili ya kumbumbusha mambo mbalimbali awapo ulingoni, amesema kwa sasa Watanzania wategemee furaha kutoka kwake kwani mchezo anaocheza ni mgumu sana na yeye amejizatiti kuleta mafanikio kwa taifa zima la Tanzania
0 comments:
Post a Comment